Kaimu Rais kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini Agapeter Basil amewataka wanawake kuingia katika mchezo huo ili kuleta chachu ya ushindani katika anga za kitaifa na kimataifa.
Akizungumza wakati wa kufungua kozi ya waamuzi wa ngumi za kulipwa nchini yaliyofanyika mjini Morogoro Basil amesema kuwa bado idadi ya wanawake Ni ndogo ikilinganishwa na wanaume katika mchezo wa masumbwi hivyo Ni fursa kwao kuendelea kujitokeza ili kuleta ushindani
Anasema katika mafunzo hayo jumla ya wanafunzi wa ukocha 33 wanachukua mafunzo wakiwemo wanaume 29 na wanawake 4 idadi ambayo ni ndogo .
Kwa upande wake katibu wa Chama Cha ngumi mkoa wa Morogoro Joseph Ngalawa amesema lengo la kuanzisha kozi hiyo mjini Morogoro Ni kuleta fursa kwa vijana kupata ajira .
Ngalawa anasema kozi hiyo italeta chachu ya kukuza mchezo wa Masumbwi mkoani huo na mpango ni kuandaa mapambano ya ngumi kila mwezi katika wilaya zote za mkoa huo ili kuibua vipaji vilivyopo vijijini.
0 Comments