Wakazi wa Mji wa Shinyanga wakiwemo watumiaji wa vyombo vya moto Barabarani wamesema ajali zinazosababishwa na waendesha pikipiki za abiria maarufu Bodaboda baadhi zinazotokana na kukosa umakini pamoja na ukiukwaji wa sheria za usalama Barabarani.
Wameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti ambapo wamesema hali ya watumiaji wa vyombo vya moto kukosa umakini Barabarani imekuwa ikichangia ajali za mara kwa mara hali inayosababisha vifo na majeruhi.
Wamesema ni makosa kisheria kwa dereva kuendesha chombo cha moto huku akiwa ametumia kilevi cha aina yoyote,kuendesha mwendo kasi,pamoja na kuendesha bila kuchukua tahadhari.
Wameliomba Jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani kuendelea kutoa Elimu sahihi juu ya sheria na kanuni za usalama Barabarani pamoja na matumizi sahihi ya alama za Barabarani ili kuzuia ajali na majeruhi.
Wananchi hao wamesema kumekuwa na ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na Watumiaji wa vyombo vya moto wasiozingatia Sheria za usalama Barabarani.
0 Comments