Header Ads Widget

SETO MKOMBOZI KWA WAPANGAJI

 




ILI kuhakikisha changamoto za wapangaji wa nyumba, vyumba, hoteli pamoja na mashamba zinapatiwa ufumbuzi, vijana wabunifu wa kitanzania wamekuja suluhu ya changamoto hiyo.


Franki Mwandi ni Mkurugenzi wa web ya Seto Dalali ambayo inaendeshwa kwa mfumo wa kidigital amesema mfumo huo unakuja kuleta ahuweni kwa wapangaji ambao wameumizwa kwa muda mrefu na madalali wa mtaani.


Mapema leo hii, akizindua mfumo huo amesema kuwa, watu wengi waliokuwa wakitafuta nyumba za kuishi mara nyingi hujikuta wakipoteza pesa nyingi bila kupata sehemu nzuri wanazozihitaji, kutokana na aina ya watu wanayokutana nayo.



"Sisi ni vijana wa kitanzania ambao tumetoka vyuoni, tumeamua kujikusanya pamoja tuweze kujiajiri na kuisaidia jamii, ambapo web hii tulioizindua leo inakwenda kuwa mkombozi kwa wapangaji wote"amesema Mwandi.


Ameongeza kuwa, mfumo huo wa kidigital utatumika ndani na nje ya nchi ikiwemo Rwanda, Uganda ambapo utakwenda kuokoa muda, gharama kubwa, wizi, kutapeliwa wakati wa kutafuta mahali pa kuishi ikiwemo hoteli nyumba za kupanga na kumbi.


Aidha amesema wateja wa nyumba na wamiliki wa nyumba watapata faida kwa kuokoa gharama ya dalali ya mwezi mzima na mmiliki wa nyumba nae atapata faida kwa kutumia huduma hiyo ya http://www.seto.co.tz.



Naye, Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya wavesleek wakili Hamza Jabir amesema kujiunga na kampuni hiyo kutasaidia mmiliki wa nyumba kuweza kupata pesa yake moja kwa moja kutoka kwa mpangaji ama mtu aliyempa idhini ya kusimamia nyumba yake.


"Nawaomba watanzania wenzangu kutuunga mkono kwa kutusapoti kwa kujisajili katika app yetu Seto Dalali halali wa kidigital asiyelala Ili kuweza kurahisisha huduma za kupata hoteli,vyumba, nyumba na hata mashamba kwa mfumo wa kidigital"amesema wakili Hamza.



Aidha, amesema huduma hiyo ni utatuzi wa gharama za nyumba kwa wapangaji ambazo hutozwa pindi wanapotafuta nyumba ambapo kupitia huduma hiyo watatoa tu shilingi elfu kumi na mmiliki wa nyumba atapata shilingi elfu sita.


Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Serikali (ICT) Commission Haji Lunga amesema Serikali itaendelea kutoa ushauri na ushirikiano kwa vijana wowote watakao jiajiri hasa kwa mfumo wa Tehema.


Hata hivyo, amewapongeza vijana hao kwa ubunifu wa mfumo huo wa seto kwa kutumia ubunifu wao wataisaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hususani katika utafutaji wa nyumba.


"Nitoe wito kwa vijana wenye mawazo kama haya na mtazamo kama huu kujitokeza kwa wingi ili kutatua changamoto zinazoikabili jamii kwa sasa, kwani vijana hawa wameonesha uthubutu kwa kuanzisha mfumo wa kidigital ambao umekua Suluhu ya changamoto za wapangaji"amesema Lunga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI