Header Ads Widget

SGA SECURITY YATOA MSAADA

 


Kampuni ya ulinzi ya SGA security mkoani Kilimanjaro imetoa masimtenk mawili  yenye Lita za ujazo elfu mbili kwa jeshi la polisi ajili ya matumizi ya jeshi Hilo.


Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema kuwa   wamekuwa wakishirikiana na kampuni hiyo kuhakikisha kwamba ulinzi na usalama unakuwepo kwenye nchi.


Aidha amesema kuwa kutokana mchango mkubwa walionao kwa jamii kampuni hiyo imewiwa kutoa masimtenk hayo mawili. 


Katika hatua nyingine amewata wote wanaomiliki silaha kinyume Cha Sheria kuhakikisha wanasalimisha silaha za aina zote  kama waziri wa Mambo ya ndani ya nchi alivyotoa maelekezo,kwani bàada ya mwezi mmoja msako mkali utafanyika kuwabaini wote wanomiliki silaha kinyume Cha Sheria ya nchi.


"Hapa tuna mapori ya kinapa mkomanzi yawezekana labda zamani watu wanatumia silaha za jadi  kuwindia wanyama ,Sasa Ile ni kinyume Cha Sheria silaha yeyote uliyonayo inatakiwa ihakikiwe"Alisema Maigwa.



Amesema kuwa kuelekea siku ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani itakayofanyika Arusha amewataka madereva kuweka stika kwenye magari ili kuepusha usumbufu pindi watakapokaguliwa.


Kwa upande wake meneja wa Kanda ya Kaskazini kampuni hiyo  Victa Mkonyi amesema kuwa wamekuwa wadau wakubwa wa jeshi la polisi kwani wamekuwa wakiwalea katika majukumu Yao ya kazi.


"Hii ni kurudisha Fadhila kwani jeshi la polisi limekuwa na mahitaji mbalimbali ,na sisi tunangalia pale tunapoweza kulingana na kipato chetu kuweza kuwasaidia ,na tunawapa pia hamasa wadau wengine wa ulinzi wakiwepo makampuni mengine kufanya hivyo Kama tunavyafanya sisi,kwani ni namna pia ya kusaidia jeshi la polisi liendelee kufanya kazi zake kwa ueledi "Alisema Mkonyi.


Hata hivyo amesema kuwa wataendelea kushirikiana na jeshi hilo la polisi kwa lolote ambalo linatokea watahakikisha wanakuwa pamoja.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Simon Maigwa akipokea masimtenk mawili yenye ujazo wa Lita 200 kutoka kampuni ya ulinzi ya SGA

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI