Header Ads Widget

SERIKALI IMEOKOA ZAIDI YA SH.BILIONI 19 KWA WATUMISHI HEWA 19708.



Teddy Kilanga, Arusha


Serikali imeokoa zaidi ya sh.bilioni 19 baada ya kuwaondoa watumishi hewa 19708 kwenye orodha ya malipo ya mishahara kati ya waliopo 535770.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Waziri wa ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora,Mohamed Mchengerwa alisema watumishi 15578 wameondolewa kazini kutokana na kubainika kughushi vyeti vya kufaulu katika mitihani yao ya kidato cha nne,sita na ualimu.



"Ningependa kusisitiza kuwa hakuna masamaha wowote uliotolewa na wizara yangu kuhusu watumishi wenye vyeti vilivyoghushiwa au kuhusu watumishi waliotoa taarifa za uongo katika kumbukumbu zao rasmi za kiutumishi kwani serikali haijatoa kibali cha kuwarejesha kazini watumishi hao,"alisema Waziri huyo.



Waziri Mchengerwa alisema kwa msingi huo msamaha ulitolewa na serikali ni kuwalipa mafao na stahiki au kuwarejesha kazini hauwahusu watumishi waliondolea kazini baada ya kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo kwani utaratibu wa kushughulikia suala hilo ulishatolewa hapo awali na serikali na haujabadilika.


Waziri huyo alisema watumishi 4380 waliondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kimakosa iliwarejesha kazini ikiwa idadi hiyo inajumuisha watendaji wa kata,mtaa na kijiji wapatao  3114,ikiwa zaidi ya watumishi 1643 tayari wamesharejeshwa kazini na serikali imeshawalipa takribani sh.bilioni 2.6 na uhikiki wa madai wa watumishi waliobaki unaendelea.


"Pamoja na kuwarejesha watumishi hao kazini pia serikali ilitoa msamaha watumishi waliondolewa kazini kwa kukosa sifa ya elimu ya kidato cha nne na baadaye wakajiendeleza na kupata sifa tajwa hapo juu hadi kufikia Desemba 2020 ambao hawakudanganya,"alisema Waziri huyo.


Pia alisema msamaha huo wa serikali uliwahusu watumishi waliojipatia vyeti vya elimu ya kidato cha nne ambao hawakudanganya katika taarifa zao wala hawakubainika kughushi vyeti.


Mchengerwa alisema pamoja na jitihada hizo za serikali hapakuwa na utaratibu bayana wa kushughulikia haki stahiki za watumishi waliondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kutokana na kuajiriwa  bila ya kuwa na cheti  cha ufaulu wa elimu wa kidato cha nne.


"Hivyo kutokana na ombwe hilo mnamo mei 7,2021 Rais  wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani alielekeza kuwa watumishi wote waliondolewa kazini kwa kukosa sifa ya kuwa na elimu ya kidati cha nne wapatiwe stahiki zao na waajiri na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu,"alisema.


Aliongeza kuwa ufafanuzi wa waziri ulilenga kutoa taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa maelekezo  hayo ya serikali kwa kundi la watumishi waliondolewa kazini kwa kukosa sifa hiyo ni walioajiriwa kuanzia mei 20,2004 na si kuwarejesha kazini watumishi waliondolewa kazini baada ya kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo katika kumbukumbu zao rasmi za kiutumishi.


Hata hivyo alisisitiza kuwa   msamaha uliotolewa na serikali wa aidha kuwalipa mafao na stahiki au kuwarejesha kazini hauwahusu watumishi waliondolewa kazini baada ya kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo hivyo msimamo wa seikali juu yao haujabadilika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI