Header Ads Widget

DC KAPANGE AKAGUA UJENZI WA MADARASA FEDHA ZA UVIKO 19.



MKUU wa Wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange Jana amekagua hatua za ujenzi wa Madarasa katika shule za Sekondari Bariadi, Ng'wang'wali na Chenge kupitia fedha za Uviko-19.


Katika ukaguzi huo, Mkuu huyo wa wilaya pia alitumia nafasi hiyo kuzijengea uwezo kamati za ujenzi za shule ili waweze kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi.



Amezitaka kamati za ujenzi kuijulisha jamii/wananchi juu ya neema ya serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na na Rais Samia Suluhu Hassan kwa wana Bariadi.



Pia aliwasisitiza wajenzi kuzingatia vipimo vyote vinavyotakiwa kufanyika kufuatwa ikiwa ni pamoja na kina cha msingi na uwiano wa mchanga na saruji kuzingatiwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI