Header Ads Widget

SAIF AL -ISLAM GADDAFI MTOTO WA KIUME WA KIONGOZI WA ZAMANI WA LIBYA KUGOMBEA URAIS


Saif al-Islam Gaddafi anatafutwa na mahakama ya kimataifa kwa uhalifu wa kivita na ni nadra kuonekana hadharani (picha ya kumbukumbu)

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Saif al-Islam Gaddafi anatafutwa na mahakama ya kimataifa kwa uhalifu wa kivita na ni nadra kuonekana hadharani (picha ya kumbukumbu)

Mwana wa kiume wa marehemu kiongozi wa Libya Muammar al-Gaddafi amejisajili kama mgombea wa kwanza wa urais wa moja kwa moja katika uchaguzi wa urais wa mezi ujao.

Saif al-Islam Gaddafi wakati mmoja alitarajiwa kuwa mrithi wa baba yake, lakini hatua yake ya kuunga mkono msakao wa kikatili dhidi ya waandamanaji mika 10 iliyopita ilimchafulia sifa.

Tangu kuibuka kwa maandamano ya mwaka 2011 ya kupinga serikali, Libya imekumbwa na mzozo.

Makundi ya kutetea haki yameelezea wasiwasi wa kuhusu uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Disemba 24, ikiwa utakuwa huru na wa haki.

Nchi zenye uwezo mkubwa duniani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wameonya kwa mtu yeyote atakayejaribu kuvuruga au kufanya udanganyifu atakabiliwa na vikwazo.

Picha na video zinazosambazwa mitandaoni zinamuonesha Saif al-Islam Gaddafi akiwa kwenye bango la uchaguzi, akisaini makaratasi ya uchaguzi.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

1px transparent line

Akiwa na ndevu na mavazi ya kitamaduni ya Libya, alihutubia kwa kunukuu aya za Quran zilizotafsiriwa kama, "hukumu baina yetu na watu wetu kwa haki".

"Mungu daima anashinda katika kusudi lake," alisema pia, akinukuu sura nyingine ya kitabu kitakatifu cha Waislamu, na kuongeza kutoka sehemu nyingine - "hata kama makafiri wanachukia".

Ni taswira tofauti kabisa na ile aliyoitoa kabla ya ghasia zilizomwangusha babake mwaka wa 2011.

Baada ya mwisho wa utawala wa kikatili wa Muammar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi mwenyewe alikamatwa na wanamgambo.

Alizuiliwa kwa miaka sita, kupewa hukumu ya kifo ambayo baadaye ilibadilishwa

Bw Gaddafi bado anatafutwa kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, lakini hatua kwa hatua amejitokeza tena hadharani, ikiwa ni pamoja na kupitia mahojiano na New York Times kutoka kwenye jumba lake la kifahari huko Zintan mapema mwaka huu [paywall].(CHANZO BBC )

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI