Header Ads Widget

PINDA AKABIDHI MIFUKO 3000 YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI WA OFISI ZA CCM BARIADI.



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu Mhandisi Kundo Andrea Mathew amekabidhi mifuko ya Saruji zaidi ya 3000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kata 31 za jimbo hilo akitekeleza ahadi aliyoitoa mapema baada ya kuchaguliwa.



Mifuko hiyo imekabidhiwa leo na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mizengo Kayanza Peter Pinda mjini Bariadi ambapo kila kata imekabidhiwa mifuko ya saruji 100, mashine moja ya kufyatulia tofali ambapo pia Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Bariadi imekabidhiwa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa jumuiya hiyo.



Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Bariadi na mkoa wa Simiyu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI