Manchester United wanakabiliwa na changamoto msimu huu , baaada ya kuanza kampeni yao kwa mguu mzuri.
United wana alama nne katika mechi sita walizocheza katika Ligi ya Premia na wako nambari sita katika jedwali la msimamo wa ligi wakiwa na alama 17.
Klabu hiyo ilipoteza mechi yake dhidi ya Aston Villa na Liverpool 5-0 na kufungwa mabao 2-0 na Manchester City Jumamosi iliyopita katika michuano ya Ligi ya Primia.
United tayari wameondolewa katika michuano ya Kombe la Carabao na wa pili katika Champions League, nyuma ya Villareal.
Ikiwa United hawatafuzu kwa Champions mwaka 2022/23, Ronaldo huenda akahamia klabu nyingine.
Kulingana na Express, Ronaldo atahitaji kuondoka Old Trafford ikiwa hali ya klabu hiyo haitabadilika.
Nahodha huyo wa Ureno, ambaye ana kiu cha kushinda vikombe na mataji binafsi, hangelipendelea kusalia katika klabu ambayo haijashinda makombe kwa muda mrefu, baada ya miaka mingi ya kurudishwa nyuma na hilo.
Katika mahojiano ya awali, Ronaldo alisema wazi kuwa anarejea katika Ligi ya Primia kushinda mataji na kukamilisha taaluma yake soka.
"Kama nilivyosema nimekuja kushinda vikombe ,"aliambia Sky Sports wakati alipojiunga na United msimu huu.
"Manchester United nembo ya kushinda mataji, na sikurudi kama mtalii.
"Nimewafahamisha kuwa naendelea vyema katika klabu. "Wana wachezaji wengi vijana wenye vipaji. Nilirudi kushinda mataji na kuimarisha timu na kuelekeza katika njia mpya."Chanzo BBC






0 Comments