MKUU wa jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefanya uhamisho na mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa nchini.
Taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa leo Novema 10 2021 kupitia msemaji wa polisi inaeleza kuwa waliohamishwa ni aliyekuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa kamishina msaidizi wa polisi (ACP) Juma Bwire ambaye amehamishiwa makao makuu ya polisi kamisheni ya upelelezi wa makosa ya jinai na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa afisa Mnadhimu wa mkoa huo kamishina msaidizi wa polisi (ACP) Alan Bukumbi.
Pia aliyekuwa mkuu wa oparesheni kanda maalum ya dae Salaam Makame Hamad amehamishiwa mkoa wa Katavi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa huo kuchukua nafasi ya kamishina Msaidizi wa polisi (ACP) Benjamin Kuzaga ambaye amekwenda kuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara .
Pia aliyekuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara kamishina msaidizi wa polisi (ACP) Marisone Mwakyoma amehamishiwa makao makuu ya polisi Dodoma kuwa msaidizi wa ulinzi wa miundo mbinu muhimu ya serikali na kamishina msaidizi wa polisi (ACP) Zuberi Mwombeji sasa anakuwa mkuu wa oparesheni kanda maalum ya Dar es Salaam .
Taarifa pia imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida yenye lengo la kuboresha ufanisi katika kutekeleza jukumu la jeshi la polisi la kulinda maisha ya raia na mali zao .





0 Comments