Mwandishi wetu, Karatu
Karatu. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu amemwaga Neema Kwa wakazi wa Karatu Kwa kuwapatia sh 10.5 bilioni na kuwajengea Daraja .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa akizungumza, wakati kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala bora na Serikali ya Mitaa, ilipotembelea kijiji cha Laja kuzindua darasaja lililojengwa na TASAF na wananchi kuomba kujengewa daraja jingine ili kuondoa ya kukwama kufika eneo ya Eyasi amesema Rais amesikia kilio chao .
Mchengerwa amesema Rais Samia Suluhu anataka kuona maisha ya watanzania yanabadilika hivyo licha ya kutolewa sh 10.5 bilioni na Kupitia TASAF Sasa amekubali kuwajengea daraja Wananchi wa Karatu.
"nimeongea na Rais Samia Suluhu amekubali atajenga daraja kuunganisha Laja na Eyasi kama ambavyo mmeomba na naagiza TASAF kuanza kufanya tathimini kushughulikia suala hili "amesema
Awali Mwenyekiti wakamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za mitaa, Abdalah Chaurembo, alisema serikali kero za Wananchi wa Karatu zitafanyiwa kazi.
Aliwataka viongozi waKaratu, kushirikiana na Wananchi kubuni miradi ambayo itakwenda kutatua kero zao.
Awali Mbunge wa Karatu, Daniel Awakie amesema, wilaya yaKaratu inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwepo tatizo la uhaba wa miundombinu na hivyo akaomba serikali kusaidia kutatua kero.
Alisema anashukuru serikali Kwa kuendelea kutoa fedha kusaidia miradi katika wilaya hiyo nakuomba isichoke kwani wilaya bado ipo nyuma.
0 Comments