Header Ads Widget

RAIS MUSEVENI AZIDI KUUNGA MKONO UTOAJI WA ELIMU TANZANIA

Wakati Rais wa Jamuhuri ya Uganda Yoweri Museveni akihitimisha Ziara yake ya Siku Tatu Nchini Tanzania, Nchini Uganda hali sio shwari baada ya Kuenea kwa kwa habari mitandaoni za Uwanja wa Ndege wa Entebe kunyakuliwa kutoka katika Mikono ya Serikali ya Uganda kutokana na Kutolipa Deni, mwandishi wa matukio daima Adrian Audax anaripoti

Rais Museveni Aliwasili nchini Tanzania Novemba 27 na kufanya mazungumzo na Rais wa Tanzania juu ya Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga Tanzania,

Sambamba na hapo November 28, Rais Museveni alitembelea Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Kufanya mazungumzo na Wafanyabishara wa Tanzania na Uganda,

Na leo Novemba 29, Rais Museveni amewasili Chato katika Mkoa wa Geita ili kukabidhi Shule ya Msingi Museveni ambayo ilijengwa kwa Ufadhili wa Serikali ya Uganda,

Ikumbukwe kuwa Rais Museveni amejenga shule nyingine pia Nchini Tanzania ambazo ni Shule ya Msingi Nyamiyaga, pamoja na Naigamba Shule ya Msingi, hivyo Shule ya Msingi Museveni ni Shule ya Tatu kujengwa na Museveni Nchini Tanzania

Kukamilika kwa Shule hiyo, Kunafanya Mkoa wa Geita kuwa na Idadi ya shule za Misingi 52 ambazo zinafundisha kwa kutumia mtaala wa Kingereza huku shule 2 kati ya hizo zikimilikiwa na Serikali na zingine zikiwa shule za watu binafsi,


IDADI YA MAJENGO

Shule hii itachukua wanafunzi wa awali pamoja na Darasa la kwanza hadi darasa la saba na wataanza rasmi Kupokea wanafunzi Januari mwaka 2021,

Majengo yaliyojengwa na kukamilika ni katika shule hii ni Jengo la Utawala 1, Vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi 17, Maktaba 1, Vyumba vya Madarasa ya Elimu ya Awali 3 , Ofisi kwa ajili ya Elimu ya Awali 2, Matundu ya vyoo 37 na Nyumba ya walimu 1 yenye uwezo wa kuchukua familia mbili,

Pia Shule ya Msingi Museveni, Itakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi 630, na hiyo ni idadi kubwa sana ya Wanafunzi kwa Mkoa wa Geita,

SABABU ZA MUSEVENI KUJENGA SHULE HIYO

Naye Rais Museveni amebainisha kuwa Hayati Magufuli hakumuomba Kujenga shule hiyo kama watu wanavyosema bali Rais Magufuli alipendekeza wajenge Shule na kuipa Jina la Museveni,

Sambamba na hilo, Rais Museveni amesema kuwa Jina la Kijiji kutumia Lugha ya Kinyankore ambalo linatumia Nchini Uganda, pia lengo lake lilikuwa ni kuweka kumbukumbu pamoja na Undugu baina ya Tanzania na Uganda, kutokana na ukweli kwamba Tanzania inabeba historia ya Maisha yake,

Novemba 27 wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Museveni alisema kuwa Mtoto wake wa kwanza alizaliwa katika hospitali ya Ocean Road Dar es Salaam,


TAASISI YA KWANZA KUTUMIA JINA LA MUSEVENI DUNIANI

Nchi nyingi za Afrika na Ulimwengu hutumia Majina ya Viongozi kuita miradi mbalimbali ya Serikali, lakini kwa Rais Museveni imekuwa Tofauti,

Hadi sasa Nchini Uganda hakuna taasisi au Mradi unaoitwa jina la Museveni, Akizungumza wakati akikabidhi shule kwa Rais Samia amesema kuwa alikataa isiitwe jina lake kwa sababu sio mali yake,

Rais Museveni amewashukuru Watanzania kukubali Jina lake kutumika kwa mara ya kwanza katika shule hiyo, huku akimuomba Rais Samia kuona namna gani ya kuongeza shule nyingine itakayo kamilisha historia,

 

SHUKURANI ZA SAMIA KWA MUSEVENI

Katika hafla ya Makabidhiano ya shule hiyo, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amemshukuru Rais wa Uganda kwa kuwa wema wa kugharamia gharama za shule hiyo,

Huku akisema kuwa Serikali itahakikishinafanya ununuzi vifaa, pamoja na kuongeza mabweni katika shule hiyo ili kwa wanafunzi wanao kaa mbali wasipate shida,

Pia amemuomba Rais Museveni kama ikimpendeza shule hiyo ya Museveni ya Tanzania, Ipate shule rafiki Nchini Uganda kwa ajili ya kubadilishana uzoefu,

Rais samia ametumia nafasi hiyo, kuwahakikishia watanzania ambao wanahofu kuhusu tamko la Serikali, kuruhusu watoto walioacha shule kwa sababu mbalimbali, ikiwemo utoro pamoj na wanafunzi waliopata Ujauzito kurejea shuleni kuwa, Serikali imelitazama hilo na halitaathiri Shuguli za kawaida za Elimu,

 *KWA UPANDE WAKE WAZIRI WA ELIMU* 

Awali waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako, alisema kuwa Makabidhiano hayo yamefanyika muda rasmi ambao serikali inapambana kuboresha sekta ya Elimu,

Pia ametumia nafasi hiyo kueleza hali ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kuwa vipo katika hali nzuri na wana uhakika wa kupokea watainiwa wote ifikapo januari 2022,


 GEITA KUNUFAIKA NA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA 

Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule, ametoa shukurani zake kwa Rais Museveni kwa kufanya ufadhili wa kujenga shule hiyo, pia amemshukuru Rais Samia kwa ushirikiano mzuri ambao umechangia katika kujengwa kwa shule hiyo,

Sambamba na hayo amepongeza mradi wa bomba la mafuta ambao pia unapita katika Mkoa wa Geita katika Wilaya za Chato Bukombe, Geita, na Mbongwe hivyo wananchi wa Geita watanufaika na fursa zitakazotokana na mradi huo,

Rais Museveni ana historia kubwa Nchini Tanzania huku akitajwa kuwa Miongoni wa Wanajeshi walioungana na Jeshi la Tanzania ili kuondoa utawala wa Idd Amin Chini Uganda mwaka 1979


Chanzo: Ziara ya Rais Museveni Nchi Tanzania

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI