Header Ads Widget

MTAA WA BONYOKWA UNATEKELEZA MFUMO BORA WA USAFI WA MAISHA WA (TAKA SIFURI)

 



Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Balozi wa Taka sifuri nchini Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa Shaaban Maliyatabu amewataka wadau na wananchi mbalimbali nchini humo kuupokea na kuuwezesha mfumo huo ili kufikia Mitaa mingine, Kata,Wilaya,Mikoa, na kuifikia Tanzania nzima.



Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima mara baada ya kutembelewa na  wakurugenzi wa Harmony Memorial Polyclinc amesema kuwa, mfumo huo unamilikiwa na jamii ambapo miongoni mwa malengo ya mfumo ni kupunguza uzalishaji na usafirishaji wa taka kwenda dampo.



"Mfumo huu umelenga kuwasaidia wananchi katika kuweka mazingira safi ndani ya jamii, kutoa ajira rasmi kwa vijana, ni rafiki kwa afya na mazingira, chanzo cha mapato pamoja na kutenganisha taka"amesema Maliyatabu.


Aidha, amesema kupitia mfumo huo, taka zinazo kusanywa zinatenganishwa katika makundi manne ikiwemo taka azo/mboji, hatarishi, rejeshi pamoja na nyenginezo ambapo zinapofika kiwandani zinakua na matumizi kulingana na aina ya taka.



"Hakika huu ni mfumo bora wa usafi wa maisha ambao umeanzia Bonyokwa ndani ya Mtaa huu na haupo popote Tanzania, karibuni wadau na wananchi kujifunza uendeshaji wa taka sifuri"amesema Maliyatabu.


Ameongeza kuwa, taka sifuri imekua mkombozi wa Bonyokwa katika masula ya usafi na mazingira kwani kabla ya mfumo huu, watu walikua wanatupa taka ovyo,ambapo kwa sasa mazingira ya Bonyokwa yamekua mazingira kutokana na watu kuweza kuuwelewa mfumo huo.


Hatahivyo, ameishukuru Taasisi ya Nipe fagio kwa kuwa wadau namba moja katika Uendeshaji wa mfumo huo ambapo wamekua wakijitoa sana kwa hali na mali Ili kuhakikisha elimu ya matumizi sahihi ya mfumo huo inawafikia jamii.



Kwa upande wake, Mratibu wa jamii kutoka Shirika la nipe fagio Abdalla Mikulu ambae ndie msimamizi wa mfumo huo amesema kuwa, wamejipanga kupeleka mfumo huo katika mikoa tofauti tofauti kulingana wadau watakavohitaji.


Amesema kuwa, lengo la mfumo huo ni kupunguza taka kwa asilimia 80 kupelekwa dampo na badala yake zipelekwe katika mfumo rasmi wa uchakataji wa taka na kuipunguzia Serikali garama za kusafirisha kuanzia ngazi  ya Halmashauri.



"Endapo taka zinazokusanywa zitapelekwa katika mfumo wa taka sifuri zitaweza kuzalisha ajira nyingi kwa vijana kwani taka nyingi zitakwenda kurejeshwa katika mfumo rasmi na kuweza na kuisaidia Serikali"amesema Abdalla.


Grace na Christina ni wakazi wa Mtaa wa Bonyokwa wamemshukuru Balozi Maliyatabu kwa kuwaletea mfumo huo ambao kwa sasa umekua rafiki kwa familia na jamii kwa ujumla.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI