Header Ads Widget

MADIWANI KASULU WASHUHUDIA UVAMIZI HUU



Baadhi ya watuhumiwa wa ujangili waliokamatwa katika eneo hili

Baraza la madiwani wa halmashauri ya Kasulu Mkoa wa Kigoma pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo wametembelea eneo la hifadhi ya Makere na eneo la wazi la ardhi oevu ambalo limevamiwa na Idadi kubwa ya wafugaji na wakulima.Na mwandishi wetu, MDTV Kasulu


Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Elia Charles  Kagoma akiwa pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Joseph Rwiza wakizungumza baada ya kutembelea eneo Hilo Jana wameeleza kusikitishwa na uvamizi unaoendelea.


Kagoma alitaka hatua za haraka kuchukuliwa na Mamlaka husika kuweka mipaka eneo hilo kutenga eneo la hifadhi na eneo la vijiji ili iwe rahisi kuwaondoa wavamizi wote.


"Lazima kuwepo alama maalum kuzunguka eneo hili ambalo ni kitaku Cha uwindaji ili kuhakikisha uvamizi unakomeshwa"alisema


Kwa upande wake Rwiza alitaka kuwepo na ushirikiano wa kupambana na wanaojihusisha na vitendo vya ujangili katika eneo Hilo ambalo ni muhimu Kwa maslahi ya Taifa.


Wanyama waliokamatwa baada ya kuwindwa na majangili

Akizungumza na viongozi hao wa halmashauri,Meneja wa  kitalu Cha uwindaji ncha Makere na eneo la wazi uvinza,Shadrack Kagoma amesema eneo hilo Sasa Kuna ujangili kutokana na uvamizi wa watu.


"Tuna wageni wa kimataifa wa uwindaji katika eneo hili lakini shida wakifika wanakuta kitalu chetu Kuna uvamizi wa Mifugo,kilimo na majangili"amesema


Amesema wavamizi wakiwepo kutoka nchi jirani wanaingia Mifugo eneo la hifadhi na kulima na baadhi wanaojihusisha na ujangili.

Eneo la ikolojia Moyowasi-Malagarasi ni muhimu Kwa maslahi ya Uhifadhi Duniani na Taifa kwani Kuna wanyama ambao hawapatikani sehemu nyingine Duniani.

Katika eneo hili linalopakana na Ziwa Tanganyika pia Kuna ndege aina ya Korongo Nyangumi ambao hawapatikani sehemu nyingine Duniani na Kuna makundi makubwa  za Zohe statunga na Pofu.

Meneja wa kitalu Cha uwindaji Cha Makere na eneo la wazi uvinza , Shadrack Kagoma akionesha watu walivyovamia eneo la hifadhi na kulima Mpunga.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI