Header Ads Widget

SERIKALI YAIPONGEZA SOS KUFANYA MALEZI MBADALA KWA WATOTO


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Dk John Jingu akifungua semina iliyoandaliwa na Shirika lisilokuwa la Kuserikali la SOS kuhusu Malezi mbadala kwa watoto yatima na waliokwenye mazingira magumu, Dar es Salaam leo Novemba 16, 2021.


Serikali imelipongeza Shirika la SOS linalojishulisha na kulea watoto yatima pamoja na walio  kwenye mazingira magumu kupitia mradi wa familia mbadala.Mwandishi wa Matukio Daima Dar es Salaam  anaripoti 

Akifungua semina ya tathimini ya mradi wa shirika hilo jijini Dar es Salaam leo Novemba 16,2021, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii,  Dk John Jingu amesema mradi wa familia mbadala ni mzuri kwani unawezesha watoto kupata haki zote za msingi ikiwemo chakula, elimu, afya pamoja na kukulia kwenye mazingira rafiki ya kijamii.


Sambamba na hilo, Dk Jingu ameliomba shirika hilo pamoja na wadau wengine kuisaidia Serikali kwenda kuwafuatilia na kuwatamvua watoto waliopo mitaani ili waweze kusaidiwa kuweza kupata haki zao za msingi kama walivyo watoto wengine.


Pia ameitaka jamii kuwajibika hususan ndugu wa familia kuchukua jukumu la kuwalea na kuwatunza watoto wa ndugu zao ambao wanafariki dunia au kupata changamoto mbalimbali za maisha.


Alisema kwa mujibu wa Sheria, jukumu la kwanza la mzazi ni kuhakikisha mtoto anatunzwa kwa kumpatia chakula, elimu, lishe na mazingira bora ya kuishi. Lakini wazazi wanapofariki, sheria inataka ndugu wavkaribu kuchukua jukumu hilo.


"Kwa hiyo Nathan rai kwa wajomba, Shangazi, baba wadogo kutambua wajibu huo kwa toto wa ndugu zenu.


"Serikali inatambua mchango wa mashirika haya, likiwamo hili SOS, katika kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapatia malezi ya kambo. Jukumu hilo mmelitimiza vizuri na niombe na mashirika mengine yaige mfano huu.


"Niombe pia mtusaidie  kuwaendea na kuwatambua watoto waliopo mitaani ili tuweze kuwapatia malezi kwenye vituo mbalimbali na hatimaye wapate haki wanazostahili" alisema Dk Jingu.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi wa SOS, Anthony Binamungu alisema lengo la semina ya siku nne iliyoanza leo, Novemba 16,2021 itajadili na kutathimini mradi wa majaribio kati ya miradi mbalimbali ya familia mbadala  iliyoanza tangu 2017.


Alisema awali walianza na watoto 50 waliokuwa wametengana na familia zao kwa kuwawezesha kupata malezi na huduma sahihi ambapo huchukua watoto kuanzia umri wa miaka sita hadi 18 ambapo huwawezesha kupata elimu kuanzia awali hadi chuo.


"Mpaka sasa kupitia vituo vyetu mbalimbali tunao watoto zaidi ya 1000. Watoto hao ni wale waliotengana na wazazi wao, tunawapatia elimu, chakula, matibabu na wengine tunawawezesha miradi ya kujitegemea baada ya kufikisha miaka 18."alisema Binamungu.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI