Header Ads Widget

MAAFISA KILIMO BUKOBA WAMETAKIWA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA WA KAHAWA.



Na, Titus Mwombeki-MTD KAGERA.


Maafisa kilimo kutoka wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wamehaswa kutumia elimu yao kuwasaidia wakulima katika kuboresha kilimo cha zao la kahawa mkoani humo iliwaweze kufanya kilimo chenye tija katika maeneo yao.



Hayo yamesemwa na meneja wa kanda taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania kanda ya Kagera kituo cha maruku Dkt. Nyabisi Maliyatabu Ng’homa katika mafunzo maalumu  yaliyolewa na taasisi hiyo Maruku mkoani Kagera ambapo maafisa kilimo hao wametakiwa kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo hayo  kuwaelimisha wakulima wazo la kahawa waweze kufanya kilimo chenye tija. 


“ Zao la kahawa nizao mama sio kwa mkoa wa Kagera tu bali katika nchi yetu kwaujumla, mabwana shamba katika mkoa wetu wanahitaji elimu ya kutosha ili kuongezeta uelewa hasa katika zao  la kahawa kwani sio kila chuo kinafundisha juu ya kilimo cha kahawa hivyo nawaomba mabwana shamba hawa waliopa nafasi ya kupatiwa elimu juu ya namna bora ya kufanya kilimo  cha kahawa wawaelimishe wakulima katika vituo vyao vya kazi waweze kufanya ili  kilimo chenye tija”



Aidha,Dkt. ng’homa ameuomba uongozi wa mkoa wa kagera  kutumia taasisi hiyo kuwaleta maafisa kilimo ili waweze kupata ujuzi jinsi ya kuzalisha zao kahawa na jinsi ya kufanya kilimo chenye tija ili wakitoka hapo waweze kuwaelekeza wakulima katika maeneo yao ya kazi jinsi ya kufanya kilimo  bora cha zao hilo. 


Naye,Areas August Urasa wakati akiendesha mafunzo hayo amesema kuwa kilimo bora cha kahawa amewahasa maafisa hao kuwasisitiza wakulima wakahawa mkoani humo kutumia miche bora ya mibuni aina ya robusta ambayo aishambuliwi na magonjwa kirahisi.



“Wakulima wa kahawa wanatakiwa kujua mambo mbalimbali yanayohusu kilimo cha kahawa ili waweze kufanya kilimo bora na chenye tija mfano kujua aina za mbegu ambazo azishambuliwi na magonjwa kirahisi, kukufanya usafi katika shamba la mibuni ikiwemo kuongoa maotea katika mibuni, kufanya palizi shambani ili kutunza unyevu shambani, kutumia mbolea kwa kuzingatia vipimo maalumu na kuangalia hali halisi ya udongo pamoja na kupanda miti shambani ilikusaidia kutoa kivuli shambani” ameongeza Urasa.



Kwaupande wa afisa kilimo kata kashalu iliyoko wilaya Bukoba mkoani Kagera  Hamad Msuya ameishukuru taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania kanda ya Kagera kwa kuandaa mafuzo maalumu kwani yamewasaidia kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa wameisha yasahau na mengime walikuwa hawajuhi kutokana na Maendeleo ya sayansi na tekinolojia kukua na kupelekea kuvumbuliwa kwa zana mpya za kilimo na ameiomba serikali kuweka mkazo katika kilimo kwa  kuwawezesha maafisa kilimo hao vitendea kazi ili waweze kufanya kazi zao kwa urahisi.


“Tunaishukuru taasisi hii kwa kutupatia elimu hasa jinsi ya kuwaelimisha wakulima wetu  jinsi ya kufanya kilimo bora cha zao la kahawa na sisi tutaitumia vyema kuifikisha kwa wakulima hao katika maeneo yetu ya kazi pia tunaiomba serikali itusaidie nyenzo ambazo zitatusaidia kuwafikia wakulima wetu kirahisi mfano vyombo vya usafiri kwani wakulima wengi wako vijijini na maeneo mengine hayafikiki lakini  dhana za kufanyia kilimo kama vile mikasi kwetu bado ni changamoto pia, kwahiyo serikali ikitimiza hayo tunaamini kilimo cha kahawa kitaongezeka na nchi itakua kiuchumi”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI