Arusha
Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imekamilisha mapitio na kupata rasimu ya mwisho wa mkakati wa Taifa wa afya moja ambayo itakuwa kati ya mwaka 2020 hadi 2026 ambao kwa sasa upo katika hatua ya kurasimishwa kwa ajili ya kuanza kutumika
Akizungumza katika kikao kazi cha wataalamu na wadau wa afya wanaoshughulika katika utengenezaji wa mkakati wa kushughulikia Afya moja katika ukanda wa Afrika mashariki,
Naibu katibu mkuu,kutoka ofisi ya waziri mkuu,sera,uratibu na bunge,Kasper Mmuya alisema ili kupunguza magonjwa yanayoenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu,usugu wa vimelea pamoja na athari nyingine za afya mpango mkakati huo hutekelezwe katika usimamizi wa maafa na kuboresha utendaji kazi pale magonjwa ya mlipuko yanapotokea.
"Natambua wenzetu serikali ya mapinduzi ya Zanzibar chini ya uratibu na usimamizi wa ofisi wa makamo wa pili wa Rais wao wanaendelea na utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa afya moja ikiwa hatua hii inahimarisha dhamira ya serikali zetu zote mbili katika kuhimarisha ushirikiano kati ya sekta za afya ya wanyama mbalimbali,binadamu na mazingira ili kupunguza mzigo wa magonjwa yanayoenea,"alisema Mmuya.
Aidha alisema serikali kupitia ofisi ya waziri Mkuu itaendelea kuhimarisha ushirikiano huo katika eneo la uratibu na usimamizi wa maafa kwa kuzingatia dhana hiyo ya afya moja ambayo ni nyenzo muhimu ya kiutendaji inayozingatia ushirikiano katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya pamoja na kuzuia na kudhibiti magonjwa yanayoathiri afya ya binadamu ,wanyama na mimea.
Hatua ya maandalizi haya ni muhimu katika kuzuia na kupambana na magonjwa ya mlipuko yanayovuka mipaka ikiwa matukio ya hivi karibuni ya kuibuka kwa magonjwa yanayoathiri baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki ikiwemo mafua makali ya ndege nchini Uganda ambapo ilitokewa mwaka 2017.
"Lakini pia kulikuwa na homa ya bonde la ufa katika nchi ya Kenya,Rwanda na Uganda mnamo mwaka 2018 pia kulikuwa na janga la uviko 19 ambalo limeathiri nchi zote za ukanda wetu na dunia nzima pamoja na kuathiri umuhimu wa kuhimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika kupambana nayo,"alisema.
Alisema serikali ya nchini Tanzania inatambua na kuendelea kuhimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa ikiwemo eneo la kupambana na changamoto ya majanga yanayovuka mipaka.
Naye Mtaalamu wa hufuatiliaji wa vimelea sugu vya magonjwa yanayotokana na usugu ambavyo vinatokana na matumizi mabaya ya dawa ambaye pia Daktari wa mifugo,Khadija Omary alisema hali halisi ya Serikali ya Zanzibar ni nzuri kutokana na jitihada za wataalamu pamoja na mwitikiao wa viongozi kukubali kuwa na mpango mkakati wa afya moja.
"Mkakati huo bado hupo kama rasimu lakini ulishafikishwa katika hatua za juu za uongozi ili kuweza kuoitishwa na hatimaye waweze kuwa na dawati la afya moja katika masuala mazima ya kupambana na magonjwa ya mlipuko yanayovuka mipaka pia yanayoweza kutoka kwa binadamu kwenda kwa mifugo kupitia kwenye mazingira yetu,"alisema Mtaalamu huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa idara ya menejimenti ya maafa,Charlse Msangi alisema mkakati wa afya moja unalenga kuhakikisha katika ukanda wa Afrika mashariki unakuwa na utekelezaji wa pamoja katika kuzuia au kupambana na magonjwa yanayovuka mipaka.
"Uzoefu unaelezea kwamba magonjwa mlipuko hayawezi kuishia katika nchi moja hivyo nchi za ukanda wa Afrika mashariki wamekutana ili kukaa kwa pamoja ukaandaliwa mkakati ambao ni rasimu hivyo tumekaa kama nchi ya Tanzania nakuangalia ni kwa namna gani utatekelezwa lakini kwa ushirikiano wa nchi za EAC,"alisema Msangi.
Grace Sabuti kutoka shirika la afya duniani kwa upande wa nchini Tanzania alieleza kuwa dhana ya afya moja ni kuhamasisha na kuendelea kusisitiza kwamba suala la afya sio sekta moja bali ni la kushirikiana na kupunguza athari kwa mwananchi.
0 Comments