Na Mwandishi Wetu.
Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT) Imefanya Semina ya Siku Moja na Waandishi Pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuelekea kuanzishwa kwa Kituo cha Umahiri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), kijulikanacho kama Regional Flagship ICT Center (RAFIC) ambapo Dola za Marekani milioni 16 zimewekezwa katika Taasisi hiyo na Benki ya Dunia kwa lengo la kuendeleza ujuzi wa TEHAMA.
Akizungumza katika Semina hiyo, Mratibu wa mradi huo Dkt. Joseph Matiko aliongezea kuwa taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam kupitia Mradi huu inalenga kutoa elimu ya kidijitali, kuongeza udahili pamoja kuwaandaa wanafunzi waweze kujiajiri na kuajiriwa ndani na nje ya nchi.
“Kwenye huo mradi wa RAFIC moja ya mambo tunayolenga ni kutoa elimu ya kidijitali ni mradi wa miaka mitano na umefadhiliwa na Benki ya Dunia, ulianza mwaka 2019 utamalizika 2024,” Mradi utainufaisha Taasisi kwa kiasi kikubwa mno ikiwemo kuboreka kwa mbinu za ufundishaji, ikiwemo kukamilika kwa ujenzi wa jengo kubwa la kisasa , kuwepo kwa vifaa vya ufundishaji pamoja na kuongeza ufahamu wa TEHAMA kwa walimu kwa lengo la kuendana na Teknolojia ya sasa. Alimalizia Dkt. Matiko
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wahariri na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam, kwa uamuzi wa kuamua kuanza na Waandishi katika utoaji wa Elimu juu ya Mradi huu, na kuahidi kuwa watakua bega kwa bega kuhakikisha wananchi wanahabarishwa kwa kina kuhusiana na mradi huu
0 Comments