Header Ads Widget

JINSI YA KUEPUKA KUPATA UGONJWA WA KISUKARI



Maelezo ya picha,

Aina ya 1 ya kisukari hugundulika mapema wakati wa utoto au ujana. Inaweza kuhusishwa na maumbile au kusababishwa na maambukizi ya virusi

Ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanaua watu zaidi ya milioni moja kila mwaka - na mtu yeyote anaweza kuupata.

Husababishwa wakati mwili hauwezi kuchakata sukari (glucose) yote katika mfumo wa damu; matatizo yake yanaweza kusababisha mshtuko wa moyo, kiharusi, upofu, figo kushindwa kufanya kazi na kukatwa kiungo cha chini.

Ni tatizo linaloongezeka kila uchwao- wastani wa watu milioni 422 wanaishi na kisukari duniani - mara nne zaidi ya miaka 40 iliyopita, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Licha ya hatari ya ugonjwa huu, nusu ya watu walio na ugonjwa wa kisukari hawajui. Lakini mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kuzuia kupatwa ugonjwa huu.

Nini kinachosababisha ugonjwa wa kisukari hasa?

Tunapokula, mwili wetu hugawanya wanga ndani ya sukari (glucose). Homoni iitwayo insulini, inayozalishwa kwenye kongosho, kisha huelekeza seli za mwili wetu kunyonya sukari hizo kwa ajili ya nishati.

Kisukari kinatokea wakati kongosho haizalishwi au haifanyi kazi ipasavyo, hivyo kusababisha sukari kujilimbikiza katika damu.

Sugar cubes and a spoonful of sugar

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Matumizi makubwa ya sukari huongeza kiwango cha sukari kwenye damu

Je, kuna aina gani za kisukari?

Kuna aina kadhaa za ugonjwa wa kisukari.

Aina ya ya 1 ya kisukari, kawaida kongosho huacha kuzalisha insulini, hivyo sukari hujilimbikiza kwenye damu.

Wanasayansi hawajui hasa kwa nini hii hutokea lakini wanaamini kuwa inaweza kuchochewa na jeni au kutokana na maambukizi ya virusi ambayo huharibu seli zinazozalisha insulini kwenye kongosho. Takriban asilimia 10 ya watu walio na ugonjwa wa kisukari wana aina hii ya 1.

Kisukari aina ya 2 , kawaida kongosho inakuwa haitoi insulini ya kutosha au homoni haifanyi kazi vizuri.

Medical illustration of the pancreas

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Insulini ni homoni inayozalishwa kwenye kongosho ambayo huwezesha mwili wetu kunyonya sukari

Hii kwa kawaida hutokea kwa watu wenye umri mkubwa, wa makamo na wazee, lakini pia vijana ambao ni wazito na wanao kaa tu bila kuushughulisha mwili, na watu kutoka makabila fulani, hasa Asia Kusini.

Baadhi ya wanawake wajawazito wanaweza kugunduliwa kuwa na kisukari wakati miili yao haiwezi kutoa insulini ya kutosha kwa ajili yao na mtoto.

Tafiti mbalimbali zinazotumia vigezo tofauti zinakadiria kuwa kati ya asilimia 6 hadi 16 ya wajawazito watapata kisukari wakati wa ujauzito. Wanahitaji kudhibiti viwango vyao vya sukari kupitia lishe, mazoezi ya mwili na/au matumizi ya insulini ili kuizuia isiendelee kuwa aina ya 2.

Watu wanaweza pia kugunduliwa kuwa na ugonjwa wa kisukari - kwa kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu na kusababisha ugonjwa wa sukari.

Nini dalili za ugonjwa wa kisukari?

A tired doctor sleeps in a hospital armchair

CHANZO CHA PICHA,

Maelezo ya picha,

Kuhisi uchovu mwingi, kiu ya mara kwa mara na kukojoa kuliko kawaida ni miongoni mwa dalili za kisukari

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI