Header Ads Widget

NGE WAUA WATATU NA KUJERUHI MAMIA YA WATU



Nge waliosambaa kusini mwa Misri wamewauma watu watatu hadi kufa baada ya dhoruba kali kuwakimbizika katika makazi yao na kuwaleta mitaani na majumbani.

Takriban watu 450 zaidi walijeruhiwa kwa kuumwa na nge hao, afisa wa wizara ya afya alisema.

Mji wa Aswan kusini mwa Misri ndio ulioathirika zaidi na uvamizi wa nge hao, ambapo mvua kubwa ya mawe pamoja na radi katika eneo karibu na Mto Nile ilishuhudiwa siku ya Ijumaa.

Kawaida mvua kubwa ikinyesha nge husombwa kutoka kweye maficho yao na kuzagaa mtaani kama ilivyo kwa nyoka, ambao pia husombwa na maji kutoka kwenye mashimo yao.

Mamlaka nchini humo zimechukua hatua ambapo mpaka sasa dozi za ziada za kuzuia sumu zimetolewa kwa vituo vya matibabu katika vijiji vilivyo karibu na milima na jangwa, afisa wa afya aliliambia shirika la habari la Al-Ahram.

Madaktari waliokuwa wanaendelea na shughuli za kutoa chanjo sasa wamelaziika kuelekeza nguvu kutibu watu walioumwa na nge, afisa huyo aliongeza.

Watu wamehimizwa kupunguza kutembea mitaani na kukaa kwa tahadhari majumbani pamoja na kuepuka maeneo yenye miti mingi:CHANZO BBC

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI