Header Ads Widget

JESHI LA POLISI LAMSHIKILIA MTUHUMIWA MMOJA KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO.



JESHI la Polisi linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa tuhuma za kukutwa na meno mawili ya tembo.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa alisema kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.



Nyigesa alisema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikamatiwa wilayani Bagamoyo atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika ambapo watashirikiana na ofisi ya wanyamapori kujua thamani ya meno hayo.



Katika tukio lingine Jeshi hilo limekamata mabegi yaliyokuwa yakisafirishwa kama mizigo yakiwa yamejaa bhangi kilo 172, kete 272 na puli 13.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI