Hoja ya Adeladius Makwega Dodoma-WUSM.
Aliingia katika ukumbi huo saa tano na ushehe, Novemba 13, 2021 kana kwamba yeye si mtoaji wa taarifa hiyo kwa umma huku akiwa amevalia suti ya rangi samawati , suruali na koti na akivalia kwa ndani ya koti lake blauzi ya rangi nyeupe. Naibu Waziri huyu alikuwa amekata nywele zake kana kwamba ni mwanafunzi wa shule ya upili na hata alipoingia sote tuliokuwamo ukumbini hatukusima.
Hatukusimama si kwa sababu ya kumkosea heshima la hasha bali tulipitiwa na wengi wakidhani kiongozi huyu wa taifa letu alikuja kutazama kama maandalizi yapo tayari kumsubiri waziri wake.
Msimamizi wa shughuli hii sasa alisimama katika marufaa na kisemeo alipaza sauti akasema ndugu wanahabari nawajulisha kuwa mheshimwa Naibu Waziri amefika na yu tayari kuzungumza nanyi.
Hata mimi ndiyo nikasema kumbe mheshimiwa yupo tukaka mkao wa kusikiliza mafanikio ya WUSM.
Naibu Waziri Pauline Gekul alisema wazi anamwakilisha waziri wake, alitaja vizuri mafanikio ya wizara yake tangu sekta ya utamaduni akaja sanaa na akamaliza na michezo. Tamati ya yote Mheshimwa Gekul alitoa nafasi ya maswali kwa wanahabari.
Muulizaji wa kwanza alikuwa ni Ramadhani Hassan kutoka Mtanzania Digitali ambaye aliuliza maswali 7 juu ya mchakato wa vazi la taifa, muulekeo wa WUSM, namna serikali ilivyojipanga kuhusu michezo, uundelezaji wa mchezo wa soka, utaratibu wa kuingia viwanjani, mipango ya serikali katika timu za taifa hasa za michezo mingine siyo soka pekee.
Muulizaji wa pili alikuwa ni Oliver huyu ni mwandishi kutoka East AfricaniTV n& Radio yeye aliuliza juu ya namna serikali ilivyojipanga katika mchezo wa masumbwi, mavazi ya wanamasumbwi yalivyo na yanavyotia aibu taifa.
Muulizaji wa tatu alikuwa ni Evance Mhando wa TBC yeye aliuliza juu ya dawati la Kiswahili ubalozini, haki miliki kwa wasanii, mfumo wa kupata vipaji katika shule za michezo, walimu wengi wa michezo wanatoka nje ya nchi na rushwa katika michezo.
Muulizaji wa nne alikuwa ni ndugu Deus Mangale huyu anatoka Tanzanite Media yeye aliuliza juu ya kuwaondoa wavamizi katika viwanja vya Jangwali-Dar es Salaam kama ilivyokuwa zamani timu za Simba na Pan zilifanya mazoezi.
Muulizaji wa tano alikuwa ni Ahmadi Said kutoka Macho Media Oline TV yeye alitaka kujua namna serikali ilivyojipanga ili kuibua vipaji katika muziki, namna ya kuwashirikisha wasanii wakubwa na wadogo.
Muulizaji wa mwisho alikuwa ni Joji Mbale wa Azam Media yeye aliuliza juu ya mirabaha kwa kazi za wasanii, bodi ya filamu na maudhui yasiyofaa kutoka filamu za nje.
Mheshimiwa Naibu Waziri Gekul aliulizwa maswali 21 na aliyajibu yote huku akiyapokea yale maswali yaliyokuja kama ushauri kuwa na lengo ya kuishauri serikali. Kikao hiki kiliwashirikisha wanahabari karibu 45 kutoka vyombo kadhaa vya umma na binafsi.
Katika maswali hayo 21 idara ya Utamaduni waliulizwa maswali 2 (9 %)tu, Sanaa maswali 5 (24 %) na michezo maswali 14 (67 %).
Kwa tafsri ya namba hizo kiasilimia kama walivyouliza wanahabari ndiyo hali halisi ya Tanzania, Watanzania wengi wanapenda sana michezo na serikali inajitahidi kuongeza nguvu katika michezo.
Kuongeza nguvu katika michezo kunapaswa kwenda sambamba na kuongeza nguvu katika sekta za sanaa na utamaduni ambazo maswali yake yalikuwa hafifu kwa asilimia ya jumla 33 % ambapo kwa hesabu za usawa wa maswali ilipaswa asilimia 33 % iwe kwa kila sekta. Kuongeza nguvu katika utamaduni kunapaswa kuwa mara dufu, maradufu kwani ukiitazama sekta ya michezo iliyoweza kuuliza maswali mengi kwa muda mrefu imekuwa na ushirikiano wa karibu na vyombo vya habari.
Mathalani utangazaji wa michezo, kuwepo kwa vipindi ya televisheni, redio na magazeti kuwa na kurasa maalumu ya michezo kila siku. Ili utamaduni na sanaa kufanya vizuri kunapaswa kuwepo na vipindi vya televisheni, redio na kurasa maalumu katika magazeti yetu kila siku Watanzania watafahamu utamaduni na sanaa yetu kwa kina huku ukitoa ajira kwao.
Kwa sasa kidogo sanaa imekuwa ikijitahidi kufanya vizuri lakini siyo sana mathalani wasanii na vyombo vya habari wamekuwa jirani sana huku wengine wakiwa hadi na vyombo vyao vya habari wakijitangaza, wengine wakiwa na kurasa za mitandao ya kijamii nakadhalika hilo ni jambo zuri sana vipi katika ngoma zetu za asili?.
Swali ambalo kwa hakika halikuulizwa na wanahabari ni je WUSM hapo awali ilikuwa ni WHUSM serikali iliiondoa idara ya habari iliyokuwa na Idara ya Habari-Maelezo, na taasisi za Habari ikiwamo TBC na TSN, je WUSM imejipanga vipi katika matumizi ya vyombo vya habari kuvitumia katika sekta zake tatu?
Katika kulijibu swali hilo na mbinu zingine ndivyo WUSM itakavyoweza kukuza utamaduni wa Mtanzania, ndivyo itakavyoweza kukuza sanaa ya Mtanzania. Nina hakika Mheshimiwa Pauline Gekul Naibu wetu au katibu Mkuu wetu Dkt. Hassan Abbasi wakipata wasaa mkiwauliza watawajibu kwa kina.
makwadeladius@gmail.com
0717649257





0 Comments