Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) anayewakilisha mkoa wa Iringa Salim Abri Asas pamoja na Viongozi mbali mbali wa CCM mkoa wa Iringa wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa Dkt Abel Nyamahanga wameshiriki Katika Kongamano la uwekezaji sekta ya Misitu mkoa wa Iringa.
Viongozi hao ambao Leo wameungana na Viongozi wa Serikali mkoa wa Iringa pamoja na kutembelea mabanda ya maonesho sekta ya Misitu pia wameshiriki Kongamano hilo lilolofunguliwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa .
Akifungua Kongamano hilo Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepongeza mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa mkoa Queen Sendiga Kwa kuandaa Kongamano hilo muhimu Katika sekta ya Misitu na kuruhusu mkoa huo kuanzisha kituo cha uwekezaji sekta ya Misitu.
Pia Waziri mkuu ameuangiza uongozi wa mkoa wa Iringa kufanya uhakiki wa viwanda ili kuona uendeshaji wake kama Kuna malighafi wanasafirisha kwenda kuchakata nje ya nchi .
0 Comments