Wananchi mkoani Mkoani Kagera wameshauriwa kuwa wanajisomea kwani itawasaidia kupata maarifa mbalimbali yatakayo wawezesha kupambana na soko la kiushindani kutoka nchi jirani.Na,Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA
Hayo yamesemwa na katibu tawala mkoa wa Kagera Prf. Faustine Kamuzola akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali Charles Mbuge katika sherehe za maadhimisho ya kilele cha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika ngazi ya mkoa wa Kagera yaliyofanyika katika viwanja vya Rumuli Manispaa ya Bukoba na kuambatana na zoezi la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiliamali wa mkoa huo pamoja na kuwasoma wanafunzi bora walioshinda katika shindano la uandishi bora wa insha kuanzia shule za msingi na sekondari kutoka katika wilaya zote zinazunda mkoa huo.
“Tunapoendelea kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika kila Mwananchi katika mkoa wa Kagera aendelee kufanya kazi kwa bidii hiyo itamuwezesha kupata kipato chake binafsi, kaya,mkoa na taifa kwa ujumla, sasa hivi tunaishi katika ulimwengu unaoitwa ulimwengu wa maarifa kila Mwananchi anatakiwa kila siku ajiboreshe kupata hayo maarifa tusipokuwa na wananchi wenye weredi mkubwa sana hatutaweza kushindana”.
Ameongeza kuwa, kila mmoja anatambua kuwa teknolojia ya habari ndiyo inayoongoza katika kuendesha uchumi hivyo vijana wanatakiwa kuweka bidii katika masomo yao na kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali hata vile vilivyoandikwa na waasisi wa taifa hili ili kuwezasha taifa la Tanzania kuwa taifa shindani.
“Niwaombe sana hasa vijana ambao mko shuleni bado muweke bidii katika masomo ya hisabati na fizikia, pia nawasihi mjitahidi sana kuwa wabunifu na kuanza kusoma kozi za kompyuta kwani itatupelekea kuwa na taifa lenye ushindani katika TEHAMA, Taifa ambalo halitakuwa shindani katika TEHAMA haliwezi kufanikiwa kamwe, unaweza kuwa na madini pamoja na ndizi kama mnavyoona hapa ila bila kuwa washindani katika suala zima la maarifa, sayansi pamoja na ubunifu kwakweli itakuwa vigumu kushindana pia nimeagiza wanafunzi walioshinda katika uandishi bora wa insha zile insha kuchapwa na kuchapichwa katika kurasa za mitandao ya kijamii ya wilaya zetu pamoja na mkoa ikiwa ni njia mojawapo ya kutambua mchango wa vijana hawa”
Aidha, Prf. Kamuzola amemtaka mkurugezi wa wilaya ya Biharamulo kuzipa kipaumbele bidhaa zinazozalishwa wilayani humo kabla ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya wilaya hiyo pamoja na mkoa wa Kagera, agizo hilo limekuja baada ya mjasiliamali kutoka katika wilaya hiyo Stanslaus Antony anayejihusisha na uzarishaji wa Chaki katika kikundi Cha BIHARAMULO DEVELOPMENT INITIATIVE kusema kuwa katika shughuli zake amekuwa akikwama kutokana na kukosa masoko ya bidhaa yake nje na bidhaa hiyo kuwa na ubora.
0 Comments