NA MWANDISHI WETU , ULANGA MOROGORO
Halmashauri ya wilaya ya ulanga imetoa kiasi cha shilingi 138,185,000.00 na kuvikopesha jumla ya vikundi 24 vya vijana, akina mama, na walemavu wilayani hapa
Akiwakabidhi hundi yenye thamani ya pesa hiyo mkuu wa wilaya ya ulanga Ngolo Malenya amesema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuwajali watanzania hasa kwenye mikopo isiyokuwa na riba
Mh malenya amesema kuwa mikopo hiyo ni ya kisheria hivyo vikundi vilivyopata mikopo hiyo vinatakiwa kurejesha kwa wakati ili na wengine waweze kupata mikopo hiyo kama ambavyo wao walivyopewa
Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri wilayani ulanga Juma Kapilima amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa serikali ipo chini ya Samia Suluhu Hassani mikopo hiyo kwa asilimia kubwa imetolewa kwa akina mama ukilinganishwa na akina baba
Mbali na hilo Kapilima amewataka waliopata mikopo hiyo kuhakikisha wanasaidia katika ukusanyaji wa mapato kwa kufichua wale wote wenye tabia ya kutorosha mapato ili halmashauri iwze kukusanya fedha ya kutosha na kuendelea kutoa mikopo hiyo.
Jumla ya vikundi 24 vimekopeshwa pesa hiyo ambapo fedha yake imetoka katika vyanzo vya bakaa ya mwaka wa fedha uliopita 2020/2021 49,141,000.,makusanyo ya marejesho ya mikopo kiasi cha shilingi 31,500,000,na fedha zilizotengwa kutoka asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa kipindi kuanzia mwezi julai hadi septemba 2021ni shilingi 57,544,000 nahivyo kufanya jumla ya fedha kuwa 138,185,000.
MWISHO
0 Comments