Kamishna Msaidizi wa Idara ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Umma (PPP), Bashiru Taratibu, akielezea miradi ya PPP ikiwa ni fursa ya uwekezaji inayotolewa na Serikali kwa Sekta Binafsi kwa Mkazi wa Dar es Salaam, Clementi Kaaya, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa masuala ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Joseph Msumule, akitoa elimu kwa Mkazi wa Dar es Salaam, Mzee Juma Mohamed kuhusu umuhimu wa Huduma za Fedha katika ustawi wa jamii, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango
Afisa Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Crispina Nkya, akitoa elimu ya fedha kwa mkazi wa Dar es Salaam, aliyetembelea Banda la Benki hiyo, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango. Mwanaidi Araba (kulia), akitoa elimu ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Umma (PPP), kwa wakazi wa Dar es Salaam, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
0 Comments