Header Ads Widget

DC NAMTUMBO AIPONGEZA KAMPUNI YA MANTRA KWA UFADHILI WA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU .





MKUU wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Dr.Julius Ningu ameipongeza Kampuni ya Mantra Tanzania Limited inayomiliki mradi wa Urani uliopo katika mto Mkuju Wilayani humo kwa kufadhili mashindano ya mpira wa miguu kwa timu 14 za Wilayani humo....Na Amon Mtega,  _Namtumbo.


Dkt. Ningu akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo yaliofanyika katika uwanja wa michezo wa Wilaya hiyo amesema Kampuni ya Mantra imetoa ufadhili wa fedha Sh.8,000,000=(Milioni Nane) kwaajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo jezi kwa timu zote 14 katika mashindano hayo pamoja na kufanikisha kuendesha mashindano hayo.



 Mkuu huyo amesema kuwa mashindano hayo yatawasaidia vijana kuibua vipaji vyao ambavyo baadhi yao vilijificha ili kuwapatia vijana wenye vipaji vya michezo waweze kusongambele kwa kuwa michezo ni ajira.



 Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mipira wa miguu katika Wilaya ya Namtumbo Zuberi Kossa ambaye pia ni mratibu wa mashindano ya Kombe la Samia (Samia Cup) amesema kuwa mashindano hayo yanaenda sambamba na mashindano ya Kombe la Samia ambayo yenye malengo makuu ya maadhimisho ya Uhuru wa miaka 60 ya Tanzania bara na miaka 59 ya Jamuhuri ya Muungano.



 Mwenyekiti Kossa amesema kuwa kampuni ya Mantra Tanzania Limited imefadhili mashindano hayo ambayo yatakuwa na zawadi kwa timu hizo  mshindi wa kwanza itapewa sh.600,000=(Laki sita)Kombe na mpira mmoja,mshindi wa pili Sh.400,000=(Laki nne) na mshindi wa tatu Sh.300,000=(Laki tatu)huku zawadi kwa timu yenye nidhamu itazawadiwa Sh.100,000(Laki moja)ambapo mchezeji bora, mfungaji bora na golikipa bora watapatiwa zawadi Sh.25,000 (Elfu ishirini na tano)kwa kila mmoja.



  Kwa upande wake Meneja mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzania Limited Khadija Pallangyo awali akitoa taarifa amesema kuwa kampuni hiyo imefadhili mashindano hayo ikiwa ni moja ya kuendelea kujenga mahusiano na jamii pamoja kuibua vipaji vya vijana kwa njia za michezo.

  

 Pallangyo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mwendeshaji na kampuni ya Mantra amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo na masuala ya michezo ili kuendana sambamba na Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

      

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI