Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA SITA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUKWEPA KODI YA SERIKALI

MAMLAKA ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Tanga imewafikisha mahakamani wafanyabiashara sita kwa kosa la kukwepa kodi ya serikali kwa kutokutoa risiti za EFD Mashine. mwandishi wa matukio daima Oscar Assenga anaripoti kutokea Tanga

Mashauri hayo sita yanayohusisha wafanyabiashara hao  yalifikishwa kwa mara ya kwanza  mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi  Tanga ,yanayohusisha kutokutii matakwa ya kisheria ya kutumia mashine za EFD ikiwa ni pamoja na kutokutoa risiti za mauzo ambayo wanayafanya.

Mashauri hayo ambayo bado yako kwenye hatua za awali yaliahirishwa mpaka November 29 na Mengine December 7 kutokana na sababu mbali mbali na watuhumiwa wako nje kwa dhamana.

Akizungumza na waandishi wa Habari nje ya Mahakamana  Afisa Sheria kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania Octavian Joseph Chenje alisema amekuja Tanga kwa ajili ya kesi mbalimbali zinazohusiana na matumizi ya mashine za kutolea risiti yaani EFD na walikuwa na mashauri sita kwenye mahakama ya hakimu mkazi Tanga.

Alisema mashauri yenyewe yanahusu masuala la utii matakwa ya sheria ya kutumia mashine za EFD ikiwemo pamoja na kutoa risiti kwa mauzo ambayo wanakuwa wakifanya .

Aidha alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao wameomba kulipa faini kutokana na makosa yao hivyo watalishughulikia suala lao na watakaa kama TRA na waendesha mashtaka ya TRA kuweza kuona kama watafanyia kazi maombi yao au waendelee na kesi.

Mwanasheria huyo alisema aliwataka wafanyabiashara kutii sheria bila shuruti sheria ya kodi ya mwaka 2015 ya usimamizi wa kodi inamtaka kila mfanyabiashara kuwa na mashine za EFD na usipofanya hivyo ukitamatwa mkono wa sheria utachukua hatua zake.

Mtu ambaye hakutoaa risiti kwa mujibu wa sheria ni faina ya milioni 3 hadi Milioni nne na nusu au adhabu hiyo pamoja na kifungo kisichozidi miaka miwili .

Naye kwa upande wake Afisa Kodi na Msimamizi wa Kitengo cha Mashine za EFD Mkoa wa Tanga Teofil  Ngambeki alisema wanajitahidi kuwaelimisha wafanyabishara kufanya biashara zao wafuate sheria za kodi pale ambapo mtu ameuza kwa kutoa risiti.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI