Header Ads Widget

WIZARA YA AFYA NA WADAU MBALIMBALI WA AFYA WAUNGANA NA NCHI NYINGINE KUADHIMISHA SIKU YA KUNAWA MIKONO DUNIANI

 


Na Hamida Ramadhani, Dodoma


WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta zinazohusika na afya mazingira na usafi inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya kunawa mikono duniani .


Siku hiyo huadhimishwa tarehe 15 Oktoba kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha jamii kuongeza uelewa na ufahamu kuhusu umuhimu  wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kama njia madhubuti na rahisi katika kudhibiti magonjwa yanayoweza kuenezwa na mikono iliyochafuliwa na vimelea mabalimbali vya magonjwa.


Akiongea leo Oktoba 15 jijini hapa na waandishi wa habari Kaimu Mkurugezi Idara ya kinga Dkt Ahmed Makuani wakati akimuwakilisha waziri wa Afya Dkt Dorothy Gwajima amesema suala la kunawa mikono kwa maji na sabuni linataikwa kupewa umuhimu mkubwa na kuzingatiwa na jamii yote  mijini na vijijini .


“Ikumbukwe kuwa usafi wa mikono ni miongoni mwa njia muhimu zilizosaidia  kujilinda na kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (UVIKO -19) ambapo Wizara imeendelea kukumbusha suala la usafi wa mikono kila mwaka kutokana na umuhimu wake katika kuzuia na kujikinga na maambukizi ya magonjwa mengine yanayotokana na uchafu na magonjwa ya mfumo wa hewa ,”amesema Dkt, Makuani.


Aidha amesema Takwimu Kutoka shirika la afya duniani (WHO) pamoja na UNCEF zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu duniani sawa na watu 3 kati ya 5 hunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ambapo katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 15 tu ya watu hunawa mikono kwa maji na sabuni.


Ameeleza kuwa nchini Tanzania kaya zenye vifaa vya kunawa mikono kwa maji na sabuni zimeongezeka kutoka asilimia 21 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 41.8 mwezi juni 2021.


“Ongezeko hili limetokana na hamasa kubwa na elimu na elimu inayoendelea  kutolewa dhidi ya UVIKO 19 pamoja na kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira yenye kauli mbiu isemayo NYUMBA NI CHOO,”amesema Dkt Makuani.


Dkt Makuani amesema unawaji wa mikono kwa kiwango kikubwa umechangia kupunguza idadi ya watu wenye magojwa ya kuhara katika vituo vya kutolea huduma za afya.


“ Kupita mfumo wa utoaji taarifa za afya (HMIS)imeonesha kwamba idadi ya watu wenye magonjwa ya kuhara wanaokwenda kwenye vituo vya afya imepungua kwa asilimia 15 ya kutoka watu  milioni 2,630,795 mwaka 2019 hadi  milioni 2,233,332 mwaka 2020 sawa na wagojwa laki 397,464,”amesema Dkt Makuani.


Hata hivyo maadhimisho hayo ya siku ya unawaji mikono duniani yamebebwa na kauli mbiu isemayo “ Maisha yetu yapo mikononi mwetu tutembee pamoja”


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI