Wananchi mkoani Kilimanjaro wanaendelea kujitokeza katika kuchangia benki ya damu salama ili iweze kuwasaidia wahitaji waliopo katika hospitali mbalimbali hapa Nchini. mwandishi wa matukio daima Rehema Abraham anaripoti kutoka Kilimanjaro.
Hayo yamesemwa na Faisal Abubakar Faruki afisa mhamasishaji wa damu salama Kanda ya Kaskazini wakati akiwa viwanja vya Mandela vilivyopo pasua mkoani Kilimanjaro akiwa katika zoezi la kuhamasisha wananchi kuchangia damu .
Aidha amesema kuwa katika wiki ya chakula duniani wanatumia nafasi hiyo kutoa elimu na kuhamasisha wananchi wachangie damu kwa hiari ili waweze kupata damu kwa wadau mbalimbali ambao wameweza kujitokeza katika viwanja hivyo vya Mandela.
"Ukiangalia kwa siku zinavyozidi kwenda watu wanaendelea kujitokeza kuchangia damu ,hivyo damu imeongezeka ukilinganisha na siku zingine zilizopita "Alisema
Hata hivyo amesema kuwa uchangiaji wa damu kwa mkoa wa Kilimanjaro unaoneasha kuridhisha kwani wananchi wamepata elimu ya kutosha ya uchangiaji wa damu na wamejitokeza kuchangia kwa hiari.





0 Comments