Header Ads Widget

MWENYEKITI UWASA APONGEZA UTENDAJI KAZI WA WAZIRI DKT KIJAZI NA PROF SILAYO

 Mwenyekiti  wa Umoja wa Wavunaji (UWASA) wilayani Mufindi mkoani Iringa, Chesco Ng'umbi, amepongeza utendaji kazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kazi nzuri anayoifanya katika kusimamia rasilimali za taifa.


Akizungumza na Matukio Daima Media Ng’umbi amesema wizara  hiyo chini ya kiongozi wake Dkt. Ashatu Kijaji kwa kushirikiana na Prof. Dosantos Silayo imeonesha uwajibikaji na ushirikiano mzuri na wadau, hatua inayochangia uendelevu wa sekta ya maliasili na kuboresha maisha ya wavunaji

“Waziri mwenye dhamana husika kwa kweli ametutendea haki sana sisi UWASA haswa kuja kutushirikisha sisi wadau katika suala zima la kujadiliana  masuala ya Maliasili na Utalii lakini nimpongeze sana Waziri kwa hatua hii ambayo bado anaendela nayo na tunaamini atatufikisha mbali sana na kwasababu yeye amekuwa kichocheo namba moja katika kufanikisha mambo yote yanayohusiana na masuala ya misitu lakini pia nisiacha kumpongeza Prof.Dosantos Silayo yeye kwa sekta yake TFS amekuwa na usimamizi mzuri tumekwenda tukishirikiana sana kwenye shughuli zinazohusiana na misitu kwa kutupa elimu juu ya utunzaji wa miti na juu ya ufanisi wa kazi.

Aidha Ng’umbi ameiomba serikali kuweza kuwafikiria kwa ukubwa kwa suala la mikataba haswa kwa wavunaji wadogo wadogo kwa nchi zima kwa kupewa mikataba rafiki ili iweze kuwasaidia katika ukopeshaji.


“Mimi nimeiomba serikali kwenye Suala la Mikataba haswa kwa wavunaji  wadogo wadogo  nchi nzima wale ambao wanavuna kwenye misitu ya serikali basi waweze kupatiwa mikataba ili waweze kukopesheka kwasababu kwa sasaivi hatuna sehemu ya kushikia unakwenda Benki unakuwa hueleweki kwaio tumemuomba Waziri hilo na amelipokea na ameahidi kwenda kulifanyia kazi.

Pia Ng’umbi ameongeza kuwa wao kama Wavunaji wanahitaji Elimu juu ya moto kwasababu kwao limekuwa ni janga kubwa japokuwa elimu hizo zimekuwa zikitolewa lakini kwa upande wao wanaiomba serikali nguvu kubwa katika utendaji na ufuatiliaji juu ya jambo hilo.

“ Jambo jingine ambalo tumeiomba serikali ni kuongeza Elimu juu ya moto, Moto umekuwa ni janga kubwa la Kitaifa lakini waongeze elimu juu ya moto na wanafanya sana kutoa elimu lakini waongeze mipango kazi ambayo inaweza kwenda kudhibiti moto ili isiweze kuathiri miti ambayo wananchi wamepanda haswa ile miti ya watu binafsi na ya serikali na tumeomba ikiwezekana serikali ipange bajeti kabisa ambayo inaweza kwenda kusaidia pale changamoto za moto zinapojitokeza .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI