Header Ads Widget

WANAFUNZI WA DARASA LA NNE KUANZA MITIHANI KESHO


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam

Jumla ya watahiniwa 1,678,209 wa darasa la nne ambao kati yao wavulana ni 823,085 sawa na asilimia 49.05 huku wasichana wakiwa 855,124 sawa na asilimia 50.95 wanatarajiwa kuanza mitihani ya upimaji kwa siku mbili kuanzia kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NACTE), Dkt Charles Msonde amesema mitihani hiyo ya  darasa la nne utafanyika katika jumla ya shule za msingi 18,144 kwa Tanzania Bara.

Aidha, amesema kuwa, mitihani hiyo itajumuisha na mitihani ya Kidato cha pili pamoja na kidato cha nne na maalifa(QT) ambapo kati ya watahiniwa 1,678,209 waliosajiliwa kufanya mitihani ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne  Watahiniwa 1,604,505 sawa na asilimia 95.61 watafanya upimaji huo kwa lugha ya kiswahili huku Watahiniwa 73,704 sawa na asilimia 4.39 watafanya kwa lugha ya kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia.

Amesema kuwa,  watahiniwa wenye mahitaji Maalumu ni 4,548 Kati yao 722 ni wenye uoni hafifu, huku 92 ni wasioona, 1,050 wenye ulemavu wa kusikia pamoja na  2,684 ni wenye ulemavu wa Viungo vya mwili.

Kwa upande Watahiniwa wa kidato cha Pili Dkt Msonde amesema Watahiniwa 651,609 wamesajiliwa ambao kati yao wavulana ni 303,913 sawa na asilimia 46.64 huku wasichana wakiwa 347,696 sawa na asilimia 53.36 wataanza mitihani hiyo Novema 1 hadi 11.

Ameongeza kuwa, mtihani wa upimaji wa kidato cha pili utafanyika katika jumla ya shule za Sekondari 5,078 Tanzania Bara, ambapo watahiniwa wenye mahitaji maalumu ni 1,014 kati yao 479 ni wenye uoni hafifu huku 52 ni wasioona na wenye ulemavu wa kusikia 215 pamoja na 263 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili.

Akizungumzia kuhusu watahiniwa wa kidato cha nne  pamoja na Maarifa (QT) Dkt Msonde alisema wanafunzi 539,243 wamesajiliwa ambapo kati yao Watahiniwa wa shule ni 502,316 huku Watahiniwa wa kujitegemea wakiwa 36,927.

Hata hivyo, amesema watahiniwa hao wataanza mitihani kuanzia Novemba 15 hadi Disemba 2 katika jumla ya vituo vya mitihani 6,090 Tanzania bara na visiwani.

"Kati ya Watahiniwa wa shule 502, 316, wavulana ni 237,776 sawa na asilimia 47.34 na wasichana ni 264 ,540 sawa na asilimia 52.66"alisema

Ameongeza kuwa, Watahiniwa wenye mahitaji maalumu ni 1,050 na kati yao 529 ni wenye uoni hafifu huku 61 ni wasioona na wenye wa kusikia 252 pamoja na wenye ulemavu wa viungo vya mwili wakiwa 208.

Kwa upande Watahiniwa wa kujitegemea Dkt Msonde amesema  36,927 huku wavulana 15,846 sawa na asilimia 57.10  huku Watahiniwa wenye mahitaji wakiwa 6 na wenye uoni hafifu 4 na wasioona ni 2.

Alibainisha kuwa mtihani wa maarifa unajumla ya Watahiniwa 9,865 kufanya mtihani wa (QT) ambapo wanaume ni 4,443 sawa na asilimia 45.04 na wanawake 5,422 sawa na asilimia 54.96.

Aidha, amesema maadalizi ya mitihani hiyo yamekamilika ambapo baraza hilo limekamilisha kuandaa na kusambazwa kwa mitihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu upimaji na mitihani katika mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani.

Aidha baraza hilo limetoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na Halmashauri, Manispaa ,Jiji kuhakikisha taratibu za uendeshaji mitihani hiyo zinazingatiwa ipasavyo.

"Tunaziomba kamati zihakikishe kwamba mazingira ya vituo vya mitihani yapo salama,tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu'amesema Dkt Msonde.

Pia baraza hilo limewataka wasimamizi wote walioteuliwa kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu .

"Wasimamizi wanaelekezwa kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni za mitihani na miongozo waliyopewa"alisisitiza

Hata hivyo baraza hilo limewataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalumu vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote cha ufanyikaji wa mitihani hiyo.


Vilevile Dkt Msonde aliwaasa Walimu wakuu, waratibu Elimu kata na wamiliki kutojiusiaha na kupanga na Kutekeleza njama za udanganyifu kwani baraza alitasita kumchukulia mtu yoyote atakayebainika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI