Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amewataka viongozi na wanachi kuhakikisha kuwa wanatunza kikamilifu vyanzo vingi vya maji vilivyopo kwani ndivyo vinavyotoa maji kutoka mlima Kilimanjaro na kuelekea maeneo ya ukanda wa chini ambayo yanaenda kutumika katika matumizi mbalimbali ikiwemo ya nyumbani na kilimo . mwandishi wa matukio daima Rehema Abraham anaripoti kutokea Kilimanjaro
Alisema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kwanza wa jumuiya ya watumia maji mto gonna/himo iliyofanyika katika ukumbi wa chuo Cha mifugo kilacha himo mkoani Kilimanjaro.
Aidha alisema kuwa uchumi na ustawi wa kazi katika maeneo mbalimbali unategemea usimamizi mzuri wa vyanzo vya Maji vilivyopo .
"Maji yetu haya mnayoyaona hapa chanzo chake ni mlima Kilimanjaro kwa sehemu kubwa ,Kuna eneo lingine dogo ambayo ni maeneo ya muheza lakini maji mengi hususani yanayotumika kwenye kilimo Cha miwa kule kwenye kiwanda Cha tpc yale maji yanatoka mlima Kilimanjaro"Alisema Kagaigai.
Alisema kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaoharibu vyanzo vya Maji kwani Kuna Sheria inayoelekeza utunzaji wa vyanzo hivyo vya Maji.
"Kuna watu wanachimba mchanga , kokoto ,wanaangusha miti na wengine wanatupa takataka kwenye vyanzo vyetu ambayo kunapita mito, nimetoa maelekezo kwa viongozi kuanzia ngazi ya vijiji pamoja na wananchi wawe walinzi wa vyanzo hivyo vya maji kwa sababu maji ni uhai"Alisema Kagaigai.
Katika hatua nyingine alisema kuwa Serikali imeweka utaratibu wa uundaji wa jumuiya za watumia maji kwenye vyanzo mbalimbali vya maji ili kuhakikisha rasirimali na usalama wa maji unatumzwa.
Hata hivyo aliwataka bodi ya maji bonde la pangani kuhakisha kuwa wanatoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa maji kwani kuna wengine wanafanya uharibifu wa vyanzo hivyo bila kujua umuhimu wa vyanzo hivyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la pangani Segule Segule alisema kuwa maji yote yanaanzia mlimani na kwenda mijini hivyo akuna mtu anayeweza kuweka mipaka kwenye maji kwani yanakatisha mkoa na kwenda mkoa mwingine yapo maji yanayotoka Tanzania na kwenda Kenya na mengine yanatoka Kenya na kuja huku.
"Kwa hiyo serikali imeona ni busara kuyafuata yale maji na kuyagawanya kwani kama kila mtu angechagua kutumia maji yake kwenye kila mkoa kuna wengine wangekosa maji kwa hiyo ikaonekana atafutwe msimamizi wa maji ambaye hana mipaka ya kiutawala " Alisema Segule.
0 Comments