Header Ads Widget

DIT YAPOKEA WANAFUNZI WAPYA

 Na Mwandishi Wetu

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wameelezwa kuwa Taasisi hiyo imejikita katika kuandaa rasilimali watu  inayohitajika kwenye uchumi wa viwanda kama ilivyoazimiwa na Serikali. 


Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof Preksedis Ndomba alipokutana na wanafunzi hao walioripoti wiki hii, mkutano huo umefanyika Kampasi kuu ya Dar es Salaam huku wengine wa Kamasi ya Mbeya na Myunga mkoani Songwe wakifuatilia hotuba hiyo kwa njia ya video.

Prof. Ndomba amesema "naomba niwafahamishe kwamba lengo letu ni kuongeza wataalam waliobobe, wabunifu na wajasiriamali.... mkakati huu aa DIT unaenda sambamba na mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka wa mitano."



                                Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,  Prof Preksedis Marco Ndomba
                                                            

Amewaeleza kuwa mpango huo unalenga kuboresha utoaji wa mafunzo na kuongeza udahili kufikia 9000 ifikapo 2025 wataalam watakao zalishwa DIT waweze kuzalisha na kuendesha viwanda. 

Amesema DIT masomo yameweka kipaumbele katika utekelezaji wa dhana ya mafunzo viwandani katika utekelezaji wa miradi inayolenga kutatua kero za Taasisi ambapo mapendekezo ya miradi inatoka kwa wanafunzi ambao wanakuja na miradi kupita kwenye ushindani kabla ya kuchaguliwa kwa vigezo vya ushindani.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Utafiti na  Ushauri wa Kitaalam, Pro. Patrick Nsimama aliwataka wanafunzi hao kuzingatia zaidi masomo


.Prof. Patrick Nsimama Makamu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu

"Acha utani na masomo usiwe kati ya watu watakaopata aibu ya kurudishwa nyumbani, jitahidi kusoma hasa," amesema Prof Nsimama.

Mshauri wa Wanafunzi wa DIT, Yosiah Misago aliwashauri wanafunzi hao kuzingatia afya zao na kujiepusha na masuala ya mapenzi ili waweze kufikia malengo yao ya kimasomo.

                                                                   Mshauri wa Wanafunzi DIT,  Yosiah Misago

Amesema licha ya kuwa mapenzi yanaharibu dira ya wanafunzi katika kuzingatia masomo, lakini pia ni hatari kwa magonjwa ikiwa ni pamoja na Ukimwi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI