Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Nchi ya Tanzania inatarajia kunufaika kupitia maonesho makubwa ya kimatafa Expo 2020 Dubai yanayoendelea kufanyika katika falme za kiarabu yalioanza rasmi Oct 1, mwaka huu hadi March 31, mwaka 2022.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dotto James ,wakati akizungumza na waandishi wakati akitoa mrejesho kuhusu Maonesho hayo ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 191 ambazo zinashiriki.
Aidha, amesema Tanzania inatumia fursa hiyo kwa kushirikiana na Sekta Binafsi kutangaza na kutafuta masoko ya uhakika na endelevu ya bidhaa zitokanazo na mazao ya kimkakati kama vile Kahawa, Korosho, Chai, Mkonge, Karafuu,Viungo bidhaa za ngozi, Mbogamboga na Matunda.
Amesema kuwa, pamoja na mambo mengine Tanzania inatangaza miradi ya kimkakati kama mradi wa kufua wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) , Reli ya kisasa (SGR) , upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, ujenzi wa viwanja vya ndege na uimarishaji wa usafiri wa anga ambapo miradi hiyo ni kuvutio na kichocheo Cha ukuaji biashara na uwekezaji hususani katika Sekta ya za kilimo na Viwanda
Hata hivyo, amesema maonesho hayo yalianza kufanyika Octoba Mosi ambapo hadi kufikia sasa fursa mbalimbali zimeweza kujitokeza ikiwemo wadau na wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuonesha bidhaa mbalimbali kwa muda wa miezi sita .
Amesema kuwa, kwa nchi ya Tanzania imejipanga Katika kuoenesha juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali Katika kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu ambayo itaunganisha bara la Afrika na duniani kwa ujumla.
Hata hivyo, amesema Katika maonesho hayo pia lipo Banda Kuu la Tanzania ambalo linahusisha Wizara, Taasisi za Serikali na Jumuiya za Wafanyabiashara ambazo zimebeba kauli mbiu ya maonesho.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC ), Dkt Godwin Wanga amesema kuna faida nyingi kushiriki katika Maonesho hayo ikiwa ni pamoja na kuvutia wabia kwa ajili ya uwekezaji na kuendeleza Sekta mbalimbali za kiuchumi.
Amesema kuwa, wataweza kutangaza vivutio vya kitalii vilivyopo nchini na kutoa fursa kwa makampuni kujitangaza na kunadi bidhaa na huduma zinazopatikana nchini ili kupata masoko endelevu, pamoja na kujenga na kuimarisha mahusiano ya kibiashara, kiuchumi na kijamii kutoka Sekta Binafsi ya Tanzania na Sekta Binafsi kutoka nchi nyengine zinazoshiriki.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Francis Nanai, amewataka wadau wa Sekta binafsi na wafanyabiashara wote wa Tanzania kushiriki maonesho hayo kupitia program mbalimbali ambazo zimeandaliwa ikiwemo ziara za kujifunza na mikutano ya kibiashara (B2B) inayojikita katika Sekta za uwekezaji wa Miundombinu na Teknolojia .
0 Comments