Hivi karibuni magenge yamepanua ngome zao kote katika jiji kuu la Port-au-Prince
Kikundi cha wamishonari Wamarekani na watu wa familia zao ,wakiwemo watotokimetekwa nyara na genge lenye silaha karibu na mji wa Haiti wa Port-au-Prince.
Takriban watu 15 walikuwa wamepanda basi baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima, vyanzo vya usalama vya Haiti vimeviambia vyombo vya habari.
Maelezo machache yanafahamika, lakini maafisa wa Marekani walisema kuwa wanafahamu ripoti hizo.
Haiti ni mojawapo ya maenei yenye viwango vya juu zaidi vya utekaji nyara duniani, huku magenge yenye nguvu yakitumia hali ya ukosefu wa sheria nchini humo kutengeneza pesa kutokana na malipo ya kikombozi.
Tangu kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse mwezi Julai, makundi hasimu yamekuwa yakijaribu kupata udhibiti na ukosefu wa usalama umekuwa ukiendelea kuimarisha mapambano ya kila siku ya kuishi miongoni mwa Wahaiti wengi.
Wamishonari hao wa Kikristo walichukuliwa muda mfupi baada ya kuondoka katika mji wa Croix-des-Bouquets na wameendelea kushikiliwa na genge, kulingana na chanzo kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP.
Wizara ya sheri ya Haiti na Jeshi la polisi bado hawajatoa kauli yoyote kuhusiana na tukio hilo.
Serikali ya Marekani bado haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo, lakini Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imeliambia shirika la AFP kuwa imeona ripoti na kwamba usalama wa raia wa Marekani nje ya nchi hiyo ni mojawapo ya vipaumbele vyake vya hali ya juu.
Christian Aid Ministries, shirika la kidini lenye makao yake nchini Marekani, lilituma ujumbe wa saujti kwa makundi ya kidini ya Haiti kama "sala maalumu'', limeripoti shirika la habari la Associated Press limearifu.
Ujumbe huo ulisema kuwa kikundi hicho kilikuwa kinafanya kazi na ubalozi wa Marekani katika Haiti "kuona ni nini kinachoweza kufanyika" kuwasaidia watu waliotekwa nyara.
Christian Aid Ministries huwasaidia Wahaiti kwa kiwango kikubwa kupitia misaada na hutoa hifadhi, chakula na nguo kwa watoto na husaidia kufadhili elimu yao.
Magenge yenye silaha yamedhibiti wilaya masikini zadi za Haiti kwa miaka mingi. Hivi karibuni yamepanua udhibiti wao katika maeneo mengine ya jiji kuu Port-au-Prince na maeneo mengine yanayopakana na jiji hilo.
Zaidi ya visa 600 vya utekaji nyara vilirekodiwa katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2021 huku 231 wakitekwa kwa kipindi kimoja mwaka jana, kulingana na kikundi cha kiraia.
Ghasia nchini Haiti-nchi ambayo ni masikini zaidi miongoni mwa mataifa ya Amerika-zimesambaa tangu kuuawa kwa Rais Moïse na wakati wa tetemeko la ardhi lililotokea mwezi uliofuata ambalo liliwauwa watu zaidi ya 200.
Kulinga na New York Times, Wahaiti wengi wamekuwa waliitolea wito Marekani kutuma vikosi vyake nchini mwao, ombi ambalo utawala wa Biden unasita kulikubali.Chanzo BBC
0 Comments