Header Ads Widget

DKT. NDUMBARO ATAJA VIPAUMBELE VYA BILIONI 90 ZITAKAZO 'BOOST' UTALII NCHINI BAADA YA COVID 19

 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro ameelezea utekelezaji wa vipaumbele vya fedha zaidi  ya Bilioni 90.2 zitakazosaidia kuinua Maliasili na Utalii katika mpango mkakati wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO – 19 kufuatia fedha za msaada za Shirika la fedha duniani [IMF] MWANDISHI  ANDREW CHALE, MDTV  DAR ES SALAAM.



Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Dkt. Ndumbaro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za mapambano dhidi ya UVIKO na kuweza kuwa wanufaika wa fedha za IMF za kusaidia mapambano ya UVIKO 19.


"Maliasili na Utalii ni wanufaika wa mkopo huu na imeidhinishiwa kiasi cha Shilingi 90,202,345,530 [Bilioni 90.2] ambayo ni sawa na asilimia 6.9 ya fedha yote iliyotengwa kutekeleza majukumu mbalimbali ndani ya mwaka wa fedha 2021/2022. 


Tunatarajia kujikita maeneo matano ambayo yameathirika zaidi na ugonjwa wa UVIKO-19. 

Hii itasaidia kuinua utalii na kuifanya sekta hii kuendelea kuchangia katika uchumi na maendeleo ya nchi."  Alisema Dkt. Ndumbaro na kuongeza;


…nichukue fursa hii kumshukuru na kumpongeza Rais Samia, jitihada zake zilizoiwezesha Serikali kupata mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi Trilioni 1.3. kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa ajili ya Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na  Mapambano dhidi ya UVIKO-19." Alisema.


Aidha, Dkt. Ndumbaro amezitaja  taasisi zilizoathirika na mlipuko wa UVIKO 19 na kutengewa kiasi cha zaidi ya Bilioni 71, ni pamoja na TANAPA,TAWA, NCAA, TFS na NMT.


"Fedha hizi zitaenda kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 5875 katika maeneo ya hifadhi za Serengeti, Mkomazi, Tarangire, Nyerere, Kilimanjaro, Saadani na Gombe, Eneo la hifadhi ya Ngorongoro.


Misitu kumi (10)   ya hifadhi ya mazingira asilia chini ya TFS  yenyewe zitagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 23.Hatua hii itasaidia kufikika kwa urahisi kwa vivutio vya utalii na kukidhi kiu ya watalii na hivyo kuchochea shughuli za utalii    na janga la UVIKO – 19." Alisema. 


Aidha, Bilioni Moja [1], imetengwa  kwa ajili ya kuweka mifumo ya kielektroniki (Develop eletronic tracking systems)  ya ufuatiliaji wa mashine kubwa na magari katika taasisi za uhifadhi huku Bilioni 3 zikitengwa ukarabati viwanja vya ndege nane (8) katika hifadhi za Taifa za: Serengeti, Nyerere, Tarangire, Mkomazi,Saadani na Katavi.


Pia kujenga malango matano (5) ya kupokelea wageni katika  maeneo ya Likuyu Sekamaganga na  Msolwa katika hifadhi ya Nyerere, hifadhi ya Mkomazi, Mapori ya Akiba ya Swagaswaga na Kijereshi.


"Kila lango litajumuisha maegesho ya magari, ofisi, maliwato (public toilets), mtandao wa maji ambao utahusisha uchimbaji wa kisima na mitambo ya umeme wa jua, ujenzi wa nyumba za watumishi, miundombinu ya TEHAMA ya kukusanya mapato, ununuzi na  magari matatu (3) ambapo jumla itagharimu Bilioni 10,


Aidha, bilioni 21 zimetengwa kununua jumla ya seti 5 za mitambo ili kuwezesha ujenzi na ukarabati miundombinu katika hifadhi kumi na tatu (13) za Taifa za: Serengeti, Ziwa Manyara, Mkomazi, Arusha na Kilimanjaro, Burigi-Chato, Ibanda-Kyerwa, Rumanyika-Karagwe, Kigosi na Rubondo na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Tarangire na Nyerere.


Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa watanunua boti maalum yenye kioo kwa ajili ya utalii wa baharini itakayotumika katika eneo la Kilwa Kisiwani itakayo itagharimu jumla ya TZS.500,000,000.


"Kukarabati miundombinu ya utalii ikiwemo barabara na vituo vya taarifa za watalii katika mapori ya akiba 11 na mapori  tengefu sita (6) kwa ajili ya kuendeleza utalii wa picha. Wizara inategemea kutumia kiasi cha zaidi ya Bilioni 8.


"Kununua  seti za mitambo ya kujenga na kukarabati  miundombinu katika maeneo ya pori tengefu la Kilombero na  mapori ya akiba ya Mkungunero na Moyowosi. Mitambo hii itahusisha ununuzi wa gari moja la kuchimba visima, Kununua boti maalum (Amphibous boat) ya kufanya doria kwenye maeneo chepechepe/ardhioevu na mashine za kuchimba visima ambapo itagharimu zaidi ya bilioni  2.


Aidha, amesema kuwa, katika hatua ya kuimarisha udhibiti wa ubora wa huduma za utalii katika kukabiliana na janga hilo la UVIKO-19, wataweka mifumo ya kielektroniki ya kutambua, kuhakiki na  kupanga huduma za malazi katika daraja za ubora.


"Hii itasaidia kutoa mafunzo kwa wataalamu wa tathmini (Assessors), wakufunzi, walimu wa wakufunzi, na watoa huduma za malazi katika kupanga daraja za ubora, kuboresha miundombinu ya mifumo ya kielektroniki ya kukusanya mapato inayowezeshwa na mkongo wa Taifa  wa mtandao wa TTCL, Kununua mifumo (software) kwa ajili ya miundombinu ya TEHAMA, ununuzi wa magari matatu (3) kwa ajili ya kazi za udhibiti wa ubora na kujenga uelewa wa miongozo (SOPs) mbalimbali ya udhibiti wa UVIKO-19 ambapo jumla ya  kiasi cha zaidi ya Bilioni Moja zitatumika katika kutekeleza shughuli hizo." Alisema Dkt. Ndumbaro.


Dkt. Ndumbaro pia ameeleza kuwa, eneo la pili ambalo fedha hizo zitaelekezwa ni kuimarisha masoko na kutangaza utalii ambapo zaidi ya Bilioni 13, zimetengwa.


"fedha hizi zitaenda kukarabati vituo saba (7) vya Urithi wa Kiutamaduni vya Mikindani Mtwara, Tendaguru-Lindi, Magofu ya Kua-Mafia, Msikiti wa Mbua Maji Mbweni, Makaburi na Msikiti wa bandarini na Kimbiji- Dar es Salaam ambapo tumetenga zaidi ya Bilioni 2.


Pia ujenzi wa kituo cha kutolea taarifa za utalii katika hifadhi ya Taifa Burigi-Chato lango la Meja Jenerali Kijuu kiasi cha Milioni 300 kitatumika.


"Zaidi ya Milioni 568 zitatumika kununua vifaa kwa ajili ya kituo cha kutolea taarifa za utalii kidigitali ili kuwezesha utangazaji wa utalii kwa kutumia mitandao ya kijamii na tovuti (Digital Command Center) pamoja na gharama za kulipia mfumo wa kutangaza vivutio vya utalii  kidigitali.


Hata hivyo, Waziri Dkt. Ndumbaro amebainisha kuwa, katika kutanua wigo wa programu ya The Royal Tour, ni kwa kukusanya taarifa mbalimbali za utalii katika maeneo mahususi ya hifadhi, vivutio vya Utalii Tanzania bara na Zanzibar na kuweka mikakati ya kuvitangaza ndani na nje ya nchi.


"Fedha Bilioni 6 zitatumika katika Programu hii ambapo itajumuisha gharama za kuandaa na kurusha  vipindi na matangazo mbalimbali nje ya nchi hususan katika vyombo vya habari vya kimataifa kwa kuhusisha watu maarufu duniani ili kuitangaza nchi zaidi.


Pia Bilioni 4 zitatumika kuwezesha  maonesho mawili (2) ya kimataifa." Alisema.


Aidha, amesema kuwa, Eneo la tatu ambalo fedha hizi zitatumika ni kuimarisha mazingira ya biashara ya Utalii kwa kuzingatia viwango vya afya na usalama vya kitaifa na kimataifa huku kiasi cha zaidi ya Bilioni 1 zikitengwa.


"Kuimarisha upatikanaji wa chanjo na vifaa vya upimaji wa UVIKO-19 katika sekta ya utalii kwa kushirikiana na Ofisi ya TAMISEMI kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Afya ambapo Wizara itajenga uelewa miongoni mwa wafanyabiashara wa utalii juu ya miongozo ya kukabiliana na Janga la UVIKO-19 katika mikoa 26.


Aidha, eneo jingine ambalo fedha hizo zitatumika ni kushirikisha Sekta Binafsi kwa kuwajengea  uwezo wa  kukabiliana na janga la UVIKO-19 na kiasi cha zaidi ya Bilioni 1, zimetengwa.


"Zaidi ya Bilioni Moja zitagharimu shughuli za kununua na kusambaza vifaa kwa  wadau wa sekta ya utalii kwa  ajili ya kujikinga na janga la UVIKO-19 na kutoa mafunzo juu ya namna ya kutumia vifaa tiba husika. 


Kutoa mafunzo na mikakati mbalimbali kwa wadau wa sekta ya utalii katika mikoa iliyoathirika zaidi ikiwemo Mtwara, Ruvuma, Lindi, Njombe, Mbeya, Mara na Mwanza ambapo kazi hizi itagharimu kiasi cha milioni 180.


Katika eneo la tano, Dkt. Ndumbaro alisema kuwa, ni kwa kuimarisha mifumo ya kidigitali ya takwimu za utalii ambapo itakayotekelezwa ni pamoja na kuboresha mifumo ya taarifa na takwimu za watalii kwa kufanya utafiti wa matumizi ya shughuli za utalii kwa kaya ili kubaini mchango wa sekta ya utalii katika Pato la Taifa ambapo zaidi ya kiasi cha Bilioni moja [1] zimetengwa.


"Kwa ujumla Wizara imetengewa kutumia jumla ya Shilingi 90,202,345,530 katika kutekeleza maeneo hayo matano katika mpango huu."  Alimalizia Dkt. Ndumbaro.


Mwisho.

[10/17, 17:33] +255 745 594 231: Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mtoto Alberth Shija mwenye umri wa Miaka Miwili na miezi kumi Mkazi wa kitongoji cha  Imalilo kata ya kitangili Manispaa ya Shinyanga, amefariki Dunia baada ya kushambuliwa na fisi.

Kwa mujibu wa Mama mzazi wa Mtoto huyo Bi Elizaberth Charles tukio hilo limetokea jana majira ya saa moja  usiku, baada ya familia hiyo  kumaliza kula chakula cha usiku ndani ya nyumba yao, na baadaye  mtoto huyo alitoka nje lakini ghafla alisikia mwanaye akipiga kelele na alipotoka nje alikuta fisi amemnyakua akikimbia naye

Amesema baada ya fisi kumwachia mtoto huyo alipelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga lakini alifariki Dunia wakati akipatiwa matibabu.

“Ilipofika jioni muda wa saa moja mtoto aliomba chakula nikampatia akala badaye akasema mama sijashiba niongezee tena nikamuongezea chakula akala alipomaliza akanawa akatoka nje muda mfupi nikasikia mama nikakimbia kukuta fisi kamkamata nikamkimbiza alikuwa amemg’ata kwenye shingo nikaanza kupiga kelele akamuachia mtoto fisi alikimbia kidogo akaenda kusimama basi nikambeba mtoto majirani wakanisaidia kumkimbiza Hospital tumefika Hospital mtoto amefariki, naomba tu serikali itusaidie tutamaliza watuwekee ulinzi tutamaliza watoto kama kunasehemu wanajua wanapoishi wawawekee hata sumu wafe”

Baadhi ya wakazi wa kata ya kitangili Manispaa ya Shinyanga Wameiomba Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa kuchukua hatua za haraka kudhibiti fisi wanaoendelea kusababisha vifo na majeruhi hasa kwa Watoto wadogo.

Vifo vya watoto wadogo vitokanavyo na kushambuliwa na fisi vimeendelea kuchukua kasi katika mkoa wa Shinynga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI