Paul Pogba anasema Manchester United inahitaji "kiubadilisha kitu fulani " baada ya kuchapwa nao 4-2 na Leicester, ikiwa ni mara ya pili wanashindwa katika mechi za Primia Ligi.
Manchester United wamechukua pointi moja kati ya pokinti tisa ambazo walikuwa na uwezekano wa kuzipata, wakishuka hadi nafasi ya tano na hivyo kupoteza fursa ya uwezekano wa kupata taji.
Kumekuwa pia na michezo mingine ambapo walipata matokeo ambayo hayakutarajiwa katika msimu huu.
"Tumekuwa na aina hizi za mechi kwa muda mrefu na hatujawahi kupata tatizo. Tumekukubali kushindwa kirahisi na magoli ya kijinga ," Pogba aliiambia televisheni ya Sky Sports.
"Kama tunataka kushinda taji, hizi ndio mechi tunahitaji kushinda, hata kama ni nguu sana.
"Tunafahamu kuwa mashabiki walitatusukuma na kutuwekea shinikizo na tunahitaji kuwa watu wazima zaidi, tucheze kwa uzoefu na majivuno-kwa njia nzuri-kwa kuchukua mpira na kucheza soka yetu.
"Tunahitaji kupata ufungua kwa ajili ya mabadiliko haya kwasababu tulipaswa kushindwa. Sijui kama ni mawazo ya wachezaji. Tunahitaji kubadili kitu fulani. Tunahitaji kutafuta mbinu za kiakili na kimkakati kushinda.Tunapaswa kuangalia kwa misingi ya kila mmoja wet una kama timu kutatua hili."
Matokeo ya kukatisha tamaa ya hivi karibuni kwa Manchester United kulitia ukomo wa rekodi yao ya kutofungwa katika mechi 29 na miezi 20.
Timu hiyo ilishindwa kudhibiti kazi ya mchezo katikati ya bustani na kukubali kushindwa kutokana na udhaifu wa safu yao ya ulinzi.
Kama meneja Solskjaer atabeba lawama nyingi zaidi kufuatia matokeo mabaya ya Manchester united
"Ni kama tuliwazawadia kusawazisha," alisema meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer.
"La pili lilikuwa ni mchezo uliopangwa, ambalo lilitukatisha tamaa. Halafu likasawazishwa…na sekunde 10 baada ya kukubali kushindwa tena. Kwahiyo kumakinika katika nyakati kubwa, hilo ni jambo muhimu katika mechi ."
Goli la kwanza la Leicester lilitokana na mkwaju kutoka kwa Manchester United wenyewe kutoka kwenye eneo lao la penati baada ya Harry Maguire kujipata hayupo.
Meneja wa Manchester United alionekana mwenye kupoteza muda wake kiufundi katika eneo lake huku Leicester, wakionekana kulisakata dimba ipasavyo na kuiyumbisha timu ambayo ilionekana kukosa mpangilio na uongozi, ikiwa na wasi wasi na kuonekana kukabiliwa na shinikizo mchana mzima.
Kama meneja Solskjaer atabeba lawama nyingi zaidi -lakini pia wachezaji maarufu waliomo ndani ya timu hii.
0 Comments