Na Rehema Abraham,_Kilimanjaro
Shirika la floresta Tanzania linaendelea kutoa elimu kwa wakulima ya jinsi ya kutumia na kuzalisha vyakula vya asili ambavyo havina madhara kwenye mwili wa binadamu.
Akizungumza katika maonesho ya kuadhimisha siku ya chakula duniani yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mandela mkoani Kilimanjaro , mkurugenzi wa shirika hilo Richard Mhina amesema kuwa wao Kama shirika wanatoa elimu kwa jamii ya jinsi ya kutunza mazingira na kizalisha bidhaa za chakula kwa njia ambayo ni rafiki kwa afya.
"Kwa hiyo sisi Kama Floresta tunahakikisha tunatoa elimu ya kizalisha chakula Cha kutosha yenye vile virutubisho vyote vya kutosha yaani (balance diet ) na tunafanya kazi na mashule ,makanisa na misikiti."Alisema Mhina.
Ameendelea kusema kuwa katika siku ya chakula duniani wamejikita katika kutoa elimu ya matumizi ya mbogamboga na matunda .
"Tumekuja na bidhaa za mbogamboga na matunda ambayo yanaonaongeza thamani na faida kwa afya kwa sababu Leo ni siku ya chakula duniani tuuawahamasisha wakulima wetu watumie vyakula vya asili". Alisema Mhina
Ameendelea kusema kuwa wanatoa elimu shuleni ya ulimaji wa maparachichi kwani wanapotoa elimu hiyo wanafunzi hawatabaki nayo Bali wanaenda kulifanyia kazi na inakuwa hazina kwa vizazi vijavyo.
Katika hatua nyingine amesema kuwa mwitikio wa wananchi kula vyakula vya asili kwa sasa umekuwa mkubwa kwani wameelewa jinsi ya kula vyakula hivyo na kiepuka vyakula vyenye kemikali.
Kwa upande Eudia Jumbe amesema kuwa amenufaika na kilimo Cha asili kwani ameweza kulima kilimo hicho bila kutumia sumu Wala mbolea za viwandani .
"Unaweza ukachanganya mimea mitatu ukachanganya kwa pamoja na ukachanganya Majani mabichi na makavu ukayaacha kwa muda na baadae ukapata mbolea yako ya mboji ambayo unaweza kutumia kwa kuoteshea mmea wowote.
Maadhimisho ya chakula duniani yamefanyika mkoani Kilimanjaro ambapo kauli mbiu ni "zingatia uzalishaji na mazingira endelevu kwa lishe na maisha Bora".
0 Comments