NA TITUS MWOMBEKI MDTV BUKOBA
Jeshi la polisi mkoani KAGERA linamshikilia Clemence Mdende mwenye umri wa miaka 51 mkazi wa Kijiji Cha Mgajwale halmashauri ya Bukoba mkoani KAGERA Kwa kumkata mapanga mke wake Bi. Odilia Rukasi mwenye umri wa miaka 47 nakumsababishia umauti.
Tukio hilo limethibishwa na mkuu wa Jeshi la polisi mkoani KAGERA AWADHI JUMA HAJI Leo akiongea na na waandishi wa habari ofisini kwake ,ambapo amesema tukio hilo limetokea tarehe 11/10/2021 majira ya saa 08:45 mchana nyumbani kwake, na kuongeza kuwa chanzo Cha tukio ilo ni wivu wa kimapenzi.
Aidha, Bwana AWADHI JUMA HAJI ametoa wito Kwa wananchi wa mkoa huo kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi katika kuripoti vitendo viovu.
0 Comments