Timu ya mpira wa pete, kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi( Sekta ya Ujenzi), yatia fola kwa kuvuka na kuingia katika hatua ya pili ya mashindano kwa kufunga michezo yote iliyochezwa.
Katika hatua hiyo, timu ya mpira wa pete ilianza michuano kati yake na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma ( RAS-RUVUMA) kwa kuwachapa magoli 21- 14, huku Wizara ya Mambo ya Nje ikigalagazwa kwa mabao 33-21, na hapo hapo Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa Wa Mara ( RAS-MARA) ikipigwa kipigo cha mabao 22-16.
Katika mchezo mingine ya netiboli timu ya Uchukuzi waliwachapa Wizara ya Kilimo kwa magoli 20-15, ambapo washindi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 11-5; nayo Ukaguzi waliwaadhibu Tume ya Walimu kwa magoli 68-5, wakati timu ya Tarura waliwafunga Katiba na Sheria kwa magoli 22-10.
Aidha, katika michuano hiyo, Sekta ya Ujenzi inaendelea na mashindano ya awamu ya pili katika mchezo wa mpira wa pete, mpira wa miguu pamoja na kuvuta kamba kwa upande wa wanaume, huku upande wa kuvuta kamba wanawake Sekta ya Ujenzi wakiyaaga mashindano hayo.
Michuano hiyo inatarajia kufika kilele tarehe 2 Novemba, ambapo washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali vikiwemo vikombe, medali na vyeti kwa washindi wote.
0 Comments