Na Mwandishi wetu, Tabora
Tabora, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania kituo cha Tumbi (Tari) mkoani Tabora wanatarajia kuzalisha mbegu zaidi ya milioni 1 za zao la chikichi ambazo zinatarajia kusambazwa kwa wakulima wa zao hilo mkoani humo.
Kauli hiyo ameitoa Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Tari Tumbi Dr Emmanuel Mrema alisema kuwa uchavushaji ni hatua ambayo hufanywa na watalaamu hao katika michikichi.
Alisema kuwa baada ya kubaini miti mama aina ya dula kisha kuangalia mti unaofaa kwa uchafushaji kazi hiyo huanza kufanyika.
“Wakulima wanapaswa kuhakikisha kuwa wanatunza vizuri michikichi kwa kufuata malekezo ya watafiti ambapo sisi tumejipanga ili kila mkulima atakae pata mbegu hizi anapata mafunzo ya namna ya kutunza shamba” alisema Dr Mrema
Nae mkulima wa zao la chikichi mkoani Tabora Kasele Nassoro alisema kuwa uhamasishaji wa zao hilo umekuwa mkubwa hivyo kuwaongezea hamasa wakulima wa kulima zao hilo.
“Tumepata elimu ya zao la chikichi ambayo awali hatukuwa nayo nimefurahi kwakuwa nimejua natakiwa nifanyeje ili kuhudumia shamba langu sikujua kuwa kuna madhara shamba likiwa chafu lakini sasa najua nifanye nini mbegu napata wapi natakiwa kufanya maaandalizi gani?” alisema Nassoro
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora Shaban maziku alisema kuwa tunashukuru uongozi wa Tari kwakuzalisha mbegu hizi katika Wilaya yetu ni jambo zuri lenye manufaa kwa wakulima wa zao la chikichi mkoani hapa.





0 Comments