Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Mjumbe Halmashauri Kuu ya Kata Kunduchi (UWT) Twilumba Jane ameutaka Umoja wa wanawake Tawi la Tandale Kibaoni Kata ya Kunduchi kuwa na mshikamano Ili kuhakikisha Mwaka 2025 Rais wa JMT Mh. Samia Suluhu Hassan anarudi tena madarakani.
Wito huo ameutoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika Mkutano mkuu wa UWT Tawi hilo ambapo amesema kwa sasa ajenda ni moja tu ya kwenda na Rais Samia katika kuitangaza Tanzania kimataifa.
"Tumepata Rais ambae anaitangaza nchi nzuri, anaiongoza vizuri, tuna kila sababu ya kujivunia yeye hivyo tusimuangushe, iwe jua ama mvua mwaka 2025 anarudi tena kwa kishindo, ametuheshimisha wanawake"amesema Twilumba.
Ameongeza kuwa, viongozi wa matawi, na ma balozi wa shina wana kila sababu ya kuwahabarisha wananchi kuhusu miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea ili watu wafahamu kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia Pamoja na serikali yake ya awamu ya sita katika kuijenga nchi.
"Nataka niwaambie kitu kimoja hakuna jambo zuri kama kuwa na mshikamano katika kazi zenu hii itajenga upendo na mshikamano baina yenu.
Lakini kama wanachama wa CCM kuendelea kuhakikisha yote yanayoendelea katika utekelezaji wa ilani ya chama Cha Mapinduzi (CCM) yanaonekana kwa vitendo"amesema Twilumba.
Aidha, alisema endapo watafanya hamasa ya kutosha kwa kuwashirikisha wanaume na watoto wote majumbani katika kukichagua chama cha Mapinduzi wataweza kushinda.
Sambamba na kuahidi kutatua changamoto za akina mama wa UWT ikiwemo kuwapelekea Kabati la kutunzia nyaraka za jumuiya ya chama.
Kwa upande wake, Katibu wa UWT Tawi la Tandale Kibaoni, Shamim Chassama amempongeza na Kumshukuru mjumbe huyo kwa kujitoa mara kwa mara katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili uwt Tawi la Tandale na kuwakumbusha zaidi wanachama kulipia ada za uanachama ili wawe wanachama hai.
"Naahidi kwa kushirikiana na viongozi wenzangu ndani ya Tawi letu tutajipanga kuhakikisha mambo maelekezo na wito uliotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Kata ya kunduchi tunaufanyia kazi ili kuleta matokeo chanya, ushirikiano wakutosha na wanachama na ushindi kwa Rais Samia ni lazima"alisema Shamim'’





0 Comments