Na Mwandishi wetu, Tabora
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari kituo cha Tumbi wamesema kuwa mbegu bora za mahindi zinapatikana kituo ni hapo.
Ambapo wamesema kuwa ili kufanya kilimo chenye tija wakulima wanapaswa kutumia mbegu hizo zenye kuvumilia ukame na kinzani kwa magonjwa huku wakipata mavuno mengi yenye tija.
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa Tari kituo cha Tumbi Dr Emmanuel Mrema wanazo mbegu bora aina tatu zinafaa kwa mazao mbalimbali nchini.
Alisema kuwa wana uwezo mkubwa wa kuzalisha mbegu za mazao mbalimbali ambayo yatamfanya mkulima anufaike na kilimo kwa kupata mavuno mengi kwenye kila zao ambalo mbegu yake itapatikana katika kituo hicho.
“Yaani sisi katika msimu huu tumezamilia kusambaza mbegu zetu katika mikoa mbalimbali inayozalisha mahindi na kuwaelezea sifa ya mbegu hizo na namna inavyoweza kutoa mavuno mengi zaidi”
“Katika tafiti zetu tumepata mbegu aina tatu ambazo niT104, T105 na high bleed TH501 zote ni mbegu bora zinazofanya vizuri shambani na wanaponunua tunawaelekeza nini wafanye kuanzia kuandaa shamba, kupanda hadi kuvuna” alisema Dr Mrema
Nae Mkurugenzi wa Uhaurishaji Teknolojia na Mahusiano kutoka Tari Juliana Mwakasendo alisema kuwa wakulima wanapaswa kuelimishwa juu ya umuhimu wa kutumia mbegu bora za Tari.
Ndio maana tunayokauli mbiu inayosema tumia mbegu za tari ongeza tija uhakika wa chakula boresha lishe na uhakika wa kipatu kwa mtu mmoja au kaya kwakuchangia ukuaji wa uchumi katika nchi kwa hili tunapaswa kuongeza nguvu katika kutoa elimu na uhamasishaji kwa wakulima kutumia mbegu bora zinazozalishwa na taasisi yetu” alisema Dr Mwakasendo
Nae Mtafiti Kilimo Kitengo cha Uzalishaji wa mbegu Bora za Mahindi Ngakwi Meibuko alisema kuwa ili mkulima aone tija kwenye kilimo hana budi kutumia mbegu bora kutoka Tari zilizofanyiwa utafiti kwa makini na watalaamu wabobezi ambapo tunashiriki kukuongeze tija katika zao hilo.





0 Comments