Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shill Bill 5.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo Sekta ya Elimu Ilala. mwandishi wa matukio daima Fatma Ally anaripoti kutokea Dar Es Salaam
Pongezi hizo amezitoa jijini Dar es Salaam alipokua katika mahafali ya 12 ya kidato cha nne Kinyerezi Sekondari ambapo wanafunzi 456 wamehitimu, amesema Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam wameingiziwa fedha na Serikali shilingi bilioni 5.1 kwa ajili ya miradi ambapo kati ya pesa hizo shilingi mil 160 zitatumika kujenga madarasa 255 ya Sekondari .
"Halmashauri ya jiji ni kweli imepata fedha sekta ya elimu sekondari imeelekeza milioni 160 wamezigawanya katika akaunti za shule zote ili ujenzi ufanyike kwa wakati malengo ya serikali yatimie shule zikifunguliwa January wanafunzi wasome " alisema Kumbilamoto.
Alisema kuwa, Taifa lolote ili liwe na maendeleo lazima wananchi wake wasome na wilaya ya Ilala wanaunga mkono juhudi za Serikali katika mpango wa elimu bila malipo, huku akiwataka wanafunzi waliohitimu kidato cha nne wilaya ya Ilala kujiendeleza kielimu hadi vyuo vikuu, kwani elimu haina mwisho .
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Kinyerezi Sekondari Veronika Mwaisaka amesema mahafali hayo ni ya 12 jumla ya wanafunzi 456 wamemaliza shule kati ya hao wasichana 249 wavulana 207.
Aliongeza kuwa, katika shule hiyo kumekua na changamoto kubwa kuhusu walimu wa somo la Sayansi ,Hisabati, masomo ya Biashara pamoja na physical.
Ameongeza kuwa, shule ya Kinyerezi Sekondari imekuwa ikijivunia mafanikio kitaaluma kila mwaka wanafunzi wake wamekuwa wakifanya vizuri darasani .
Aidha alitumia nafasi hiyo kumpongeza Afisa Elimu Halmashauri ya Dar es Salaam Mwalimu Mussa Ally kwa uongozi mzuri wenye mafanikio sekta elimu Wilaya ya Ilala.
0 Comments