RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakati ukipigwa wimbo wa Taifa na wa Afrika Mashariki kabla ya kuaza kwa hafla ya kuwaapisha Viongozi aliowateua hivi karibuni.
Majaji wa Mahkama Kuu Zanzibar wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar na Mwanasheria Mkuu na Naibu Mwanasheria, wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar 30-10-2021.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Muumin Khamis Kombo kuwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bi. Salma Ali Hassan kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha.Bi.Mwanamkaa Abdulrahaman Mohammed kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka
BAADHI ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wanafamilia wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Jaji wa Mahkama Kuu na Mkurugenzi wa Mashtaka na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka.
0 Comments