Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wamedhihrisha ubora wao katika mchezo wa Netiboli kwa kuwashinda Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) kwa jumla ya magaoli 43-34 na kutinga nusu fainali ya Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea viunga vya Manispaa ya Mororgoro. mwandishi wa matukio daima Eleuteri Mangi anaripoti kutokea Morogoro
Timu hiyo ilitandaza mchezo safi wa kutakata na pasi fupifupi za kuonana wakiongozwa na Nahodha wao Jane Thawe ambaye wakati wote wa mchezo huo amekuwa mfungaji mahiri
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo ambayo yanazingatia na kuendeshwa kwa Sheira za mchezo wa netiboli kama yalivyotolewa maelekezo katika kanuni za mashindano ya SHIMIWI aya ya 6 timu hizo zilifika kituo cha mashindano kwa wakati ambapo kanuni hiyo inasisitiza timu kufika siku moja kabla ya mashindano kuanza na kiongozi wa timu kuripoti kwenye kituo kilichowekwa na Kamati ya Utendaji.
Timu tatu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambao wamefunga timu ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) magoli 43- 34, Hazina ambao wamewafunga timu ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa jumla ya magoli 27-20, Ofisi ya Rais Ikulu ambao walipata ushindi wa magoli 40-0 dhidi ya timu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Timu ya nne katika hatua hiyo itapatikana baada ya kumalizika mchezo dhidi ya timu za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kukamilisha mchezo wao kutoshana nguvu kwa kufungana goli 39-39.
Mechi zote za hatua ya nusu fainali inachezwa katika Uwanja wa Jamhuri uliopo manispaa ya Morogoro ambapo mabingwa katika michezo yote wanatarajiwa kukabidhiwa vikombe na zawadi zao Novemba 02, 2021 katika uwanja huo.
0 Comments