Ametoa siku 30 kwa wamiliki haramu wa silaha hizo kuzisalimisha katika vituo vya polisi, ofisi za Serikali za Mitaa na kwa Watendaji wa Kata.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) sheria ya kudhibiti silaha na risasi ya Mwaka 2015, Sura ya 223, baada ya kutangaza msamaha na usalimishaji wa silaha kwa wamiliki wa silaha kinyume na sheria, jijini Dodoma,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akimsikiliza Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo, Lebaratus Sabas
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akisalimiana na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza, wakati alipokuwa anawasili kuzungumza na waandishi wa Habari, jijini Dodoma, leo. Katikati ni naibu katibu Mkuu, ramadhani kailima, wapili kulia ni Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo, Lebaratus Sabas.
0 Comments