Mbunge wa Kilolo Justin Lazaro Nyamoga ameendelea na ziara kata ya Irole kijiji cha Lundamatwe mkoani Iringa akiwa pamoja na diwani wa kata hiyo Mhe. John Mkonda. na mwandishi wa matukio daima.
Mhe. Nyamoga ameendelea kupokea maoni na kero za wananchi ambazo kwa nafasi yake ya uwakilishi wa jimbo la Kilolo bungeni ataendelea kuyasemea na kuyafikisha mahali husika, hasa kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi.
Na kwa upande wa Elimu kwa kijiji cha Lundamatwe Mhe. Nyamoga amewaahidi kuwaunga mkono wakazi wa kijiji hicho katika ukarabati wa majengo ya shule ya msingi Lundamatwe kupitia mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo pamoja na mapato ya ndani kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Kilolo.
Pia kwenye Afya, Mhe. Nyamoga amewahakikishia wakazi wa kijiji cha Lundamatwe jengo lao la maabara atalipatia kipaumbele ili likamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.





0 Comments