Header Ads Widget

AKINA MAMA WAJAWAZITO WATAKIWA KULA VYAKULA VYENYE VIRUTUBISHO

Akina Mama wajawazito wameshauriwa kuzingatia lishe bora kwa kula  vyakula vyenye virutubisho ili kuepuka kuzaa  watoto wenye udumavu. mwandishi wa matukio daima Hadija Omary anaripoti kutokea Lindi

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi hivi karibuni alipokuwa anazungumza na wanawake wajasiliamali alipokuwa anazindua Mpango wa kukuza fursa za Biashara za ufukweni kupitia Tamasha la michezo mbali mbali ya ufukweni kwa vikundi vya wajasiliamali wa kuweka Akiba ya pesa na Kukopa (VICOBA) lililopewa jina la VICOBA FUN DAY. 

Bi Telack alitumia Fursa hiyo kuwahasa akina Mama hao kuzingatia lishe Bora pindi wanapokuwa wajawazito kwa kutumia vyakula vinavyowazunguka katika Maeneo yao.

Alisema ni Muhimu sana kwa mama kula vyakula vyenye lishe bora kwani lishe hiyo hutumika kwa Mama na Mtoto anaendelea kukua akiwa tumboni. 

"Akina mama wenzangu ngoja niwaibie siri wale wasiotaka kula vizuri ndio ambao wanazaa kila siku na matokeo yake uzaa watoto waliedumaa kimwili na kiakikili"

Telaki aliongeza kuwa kwa kawaida mahitaji ya chakula na virutubisho mwilini mwa mwanamke huongezeka wakati wa ujauzito na kadri ujauzito unavyokuwa  virutubisho hivyo hutumika kujenga mwili wa mama na mtoto.

Hata hivyo aliwataka akina mama hao kufuata ushauri wa Madaktari pia kuhusu kuwapa chakula watoto hao  baada ya kujifungua kwani hata mtoto akishazaliwa asipo lishwa vizuri pia anaweza kudumaa.

" Vifo vya watoto wachanga ni vingi kwa sababu tunawapa watoto maji wakiwa na siku moja mpaka saba na pengine ukihisi ajashiba maziwa basi unampa viuji vyepesi vyepesi  utumbo haujakomaa matokeo yake Mtoto anakufa" aliongeza Telack

Kwa upande wake Hadija Mkalindende mkazi wa Manispaa ya Lindi alisema kuwa bado Elimu ya lishe bora kwa wajawazito inatakiwa kuendelea kutolewa kwani  akina mama waliowengi wanadhani anaeweza kula lishe bora ni yule mtu mwenye uwezo wa kipato kikubwa peke yake. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI